Thursday, January 3, 2013

BREAKING NEWS, FIRE DISASTER IN SINGIDA

Maduka kadhaa ya biashara katika soko kuu la mjini Singida yameungua moto, mali nyingi zimeungua na kikosi cha zima moto kwa kushirikiana na jeshi la polisi na vikosi vingine vya ulinzi na usalama vinaendelea na jitihada za kuzima moto huo

Chanzo cha moto huo hadi sasa hakijatambulika, ingawa shirika la ugavi wa umeme Tanzania Tanesco, lililazimika kukata huduma ya umeme kwa muda na baadaye kuurejesha tena

Inahofiwa kuwa, huenda moto huo umetokana na hitilafu ya umeme

Taarifa zaidi za tukio hili pamoja na picha zitawekwa kwenye blog hii muda mfupi ujao

endelea kuwa nasi

Wednesday, January 2, 2013

SALAAM ZA MWAKA MPYA TOKA STANDARD RADIO

Wakati wa sikukuu ya Noeli na mwaka mpya mambo mengi hufanyanyika, kubwa zaidi huwa ni salaam kwa maradfiki, ndugu na hata kupeana zawadi

watumishi wa standard radio fm Singida wanatumia fursa hii kutoa ujumbe mhimu wa kutakiana heri ya Mwaka mpya.

FUATILIA SALAAM HIZI PAMOJA NA U JUMBE KUTOKA KWA WANA STANDARD

BONIFACE MPAGAPE: Uzuri na utamu wa ngoma, ingia lingoni ucheze! Shiriki kwa dhati katika kila suala linalohusu maendeleo ya jamii yako. Ninaomba ushirikiano wako ili tuweze kuleta mabadiliko katika jamii. Kheri ya Mwaka mpya 2013
 
 
 
 
 
Eufrasia mathias:Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili, fanya kazi uonje matunda ya akili yako.
It is better to  be terminated because of hardworking than to be terminated because of laziness
 
 
 
 
Edilitruda Chami: Matokeo mazuri yankusubiri wewe ,tembea na malengo,kimbia kwa kujiamini mwaka 2013,paa ukitambua kuzaliwa maskini siyo kosa lako bali ukifa maskini ni kosa lako
 
 
 
 
Moses Anthony John: Namshukuru Mungu kwa kumaliza na kuanza mwaka vizuri , kuna mengi tumekumbana nayo na bado kuna mengi tutakutana nayo, mazuri kwa mabaya ila kwa uwezo wa Mungu tutasonga,Niwatakie kheri ya mwaka mpya STAFF wote wa SR na Buhanzo enterprises na watanzania wote
 
 
 
 
Zaituni M. Kimu: Bila Mwenyezi Mungu hakuna linalowezekana,  Namshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufikia Mwaka huu 2013, Na wale ambao Mwenyezi Mungu hakupenda wafikie mwaka huu 2013 tuwaombee wawe mahala pema, Na waliokuwa wagonjwa Mungu awape afya njema na tumwombe Mungu kwa kila lililokuwa zitokwa mwaka uliopita,atufanyie wepesi katika mwaka huu mpya wa 2013
 
Gerald Joseph: Heri ya mwaka mpya mdau wa Standard Radio pamoja na wafanyakazi wote wa Standard Radio
Tusifikirie yaliyopita maana yanaumiza moyo,wala tusifikirie yajayo maana yanakatisha tamaa.Tufikirie yaliyopo na kuyafanyia kazi
 
 
Khadija Mahamba: Tumshukuru Mungu kwa kutupa nafasi tena ya kuendelea kuwepo duniani 2013 haimaanishi ambao hawajauona mwaka huu Mungu hawapendi La! Ila jiulizze utafanya yale aliyoyaagiza uyafanye hapa duniani? Namaanisha Badilika, rudi kwa Muumba wako achana na mabaya yaliyokuwa yakikupendeza fanya mazuri yampendezayo Muumba wako na wazazi wako . Endelea kusikiliza Standard radio
 
Elizabeth Mwaja: Heri ya mwaka mpya 2013, Kufika mwaka 2013 ni uweza wake Mwenyezi Mungu kwani wengi walitamani kufika lakini hawakuweza kufika kutokana na vikwazo mbalimbali kama vile maradhi, vita na ajali. Tumwombe Mungu atuvushe tena mwaka huu
 
Agnes Samweli: Namshukuru Mungu amekuwa mwema kwa Standard Radio kwani changamoto tulizokutana nazo,hatujutii, ni hali ya kawaida, hivyo nawaomba wana Standard wote tushirikiane kwa upendo wa dhati ili tuweze kusonga mbele
 
Deborah Marco: Kila mtu yupo duniani kwa makusudi kamili ya Mungu.Nawatakia mafanikio mema ya mwaka 2013 yale yote ambayo hujayatimiza 2012 uyatimize 2013
 
Joseph Monko, Nawashukuru wafanyakazi wote wa standard Radio kwa moyo tuliouonesha, tuendelee kwa moyo huohuo. nawatakia heri ya mwaka mpya
 
 
 
 
Noel Exavery: Furahini katika Bwana siku zote tena nasema furahini, upole wenu na ujulikane na watu wote
 
 
 
 
 
 
 

MRADI WA MAHUSIANO SINGIDA WAGHARIMU MIIONI 149

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Singida Non – Governmental Organizations Network (SINGONET), limetumia zaidi ya shilingi 149.8 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuimarisha mahusiano kati ya wananchi na wabunge, madiwani na watendaji wa serikali.
Hayo yameelezwa juzi na mratibu wa SINGONET, Maendeleo Makoye, wakati akitoa taarifa yake kwenye mdahalo mkubwa kwa kuimarisha mahusiano ya wananchi na wabunge,madiwani na watendaji wa serikali.
Alisema fedha hizo zilizotolewa na shirika la The Foundation For Civil Society kugharamia mradi huo, ambao umetekelezwa katika awamu nne kuanzia Septemba mwaka jana hadi Septemba mwaka huu.
Makoye alisema kuwa mradi huo ulilenga kuamsha ari ya ushiriki na ushirikiashwaji wa wananchi katika kuchambua, kujadili na kutoa mapendekezo yao juu ya mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya ya Tanzania.
Aidha alitaja malengo mengine kuwa ni kujenga na kudumisha uhusiano na ushirikiano kati ya asasi za kiraia na wananchi na kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii hasa katika upatikanajii wa huduma za elimu, afya, upatikanaji wa maji na nishati.
Katika hatua nyingine, Makoye alisema baadhi ya wabunge na Madiwani nchini, wameshindwa kuonyesha uwajibikaji wao kwa umma kama inavyotarajiwa.
Akifafanua zaidi,Makoye alisema wawakilishi hao wameshindwa kushiriki pamoja na kushirikisha jamii katika kubuni, kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango mbalimbali ya maendeleo.
“Hakuna utaratibu ulio wazi juu ya mijadala ya pamoja kati ya wananchi na wawakilishi wao. Kwa maana hiyo, wananchi hawashiriki kuchangia maoni na mawazo ambayo Mbunge au Diwani anapaswa awawakilishe katika taasisi za maamuzi”,alisema Makoye.
Mratibu huyo, alisema mapungufu hayo ya kimawasiliano, jamii imeshindwa kuwakilishwa vilivyo na matokeo yake, serikali imeshindwa kutimiza ipasavyo mahitaji halisi na matarajio ya wananchi wake.

MAMILIONI YAIBWA IDARA YA AFYA SINGIDA

Na. Halima JamalSingida KESI inayomkabili mhasibu hospitali ya Mkoa Singida na walinzi watatu wa kampuni binafsi kuhusiana na wizi wa Sh. 15,976,650, imeanza kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa, kwa mganga mkuu wa mkoa kutoa ushahidi kuhusiana na tukio hilo.
 

Mhasibu huyo, Rahel Misai na walinzi watatu wa kampuni ya ulinzi ya Yange, Athumani Yohana, Juma Shabani na Rehema Hussein walishitakiwa kwa makosa manne ya wizi wa fedha hizo, zilizohifadhiwa ofisi ya kutunzia fedha, hospitali ya mkoa Singida.

 
Akitoa ushahidi, mganga mkuu mkoa wa Singida, Dk. Dorothy Kijugu aliieleza mahakama kuwa siku hiyo saa moja asubuhi wakati anajiandaa kwenda kazini, alipigiwa simu na mganga mkuu wa kituo kuwa ofisi ya mhasibu imevunjwa na fedha zimeibwa.
Akiongozwa na mwendesha mashitaka mratibu msaidizi wa polisi Shukurani Magafu,Dk. Kijugu alisema baada ya kufika hospitalini aliwakuta askari na katika kukagua walibaini kuvunjwa kwa milango yote minne hadi kufika chumba cha kuhifadhia fedha.
Alisema, baada ya kushuhudia hali hiyo, baadaye ilibidi mkaguzi mkuu wa ndani akague kwa kina, na taarifa yake ilithibitisha kuibwa kwa kiasi hicho cha fedha. Shahidi huyo aliikabidhi mahakama kielelezo cha nakala ya ukaguzi wa tukio hilo.
Hata hivyo katika maswali dhidi ya shahidi, washitakiwa walimuuliza, anadhani tukio hilo lilitokea majira ya saa ngapi, je anawafahamu washitakiwa hao?, muda wa walinzi kubadilishana zamu na wakati wa mhasibu kuingia na kutoka kazini.
Katika majibu yake, shahidi alisema anayepaswa kujua majukumu yao ni mganga mkuu wa kituo, badala ya yeye ambaye anahusika zaidi na utawala wa mkoa mzima, ikiwemo hospitali za wilaya, na juu ya muda wa mhasibu kutoka kazini aliieleza mahakama kuwa ni saa 9:30 jioni.
Kwenye shauri hilo, washitakiwa walifanya kosa hilo julai 13, 2012 usiku, wakihusishwa na mashitaka manne, ikiwemo kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kuvunja usiku na kuiba fedha, wizi wa Sh. 15,976,650 mali ya hospitali mkoa na kosa la nne kushindwa kuzuia wizi huo.Shauri hilo limepangwa kuendelea kusikilizwa januari 3, 2013.