Tuesday, October 29, 2013

UMUHIMU WA KUCHANGIA UJENZI WA VYUMBA VYA MAABARA SHULENI

Na.Neema Mwampamba
Mkuu wa mkoa wa singida Dr Perseko Korne amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa serikali ili kufanikisha ujenzi wa maabara katika shule za sekondari
Akizugumza na standard radio ofisini kwake Dr Korne amesema ni lazima kila mzazi kuwajibika kwa kutoa mchango wa ujenzi wa maabara ili kuwawezesha wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kujengewa msingi mzuri
Aidha amesema juhudi zinafanyika ili kuhakikisha maabara za masomo ya Biology Chemia na phizikia zinakamilika katika shule zote ifikapo February 2014
Hata hivyo amewapongeza wakazi wa mkoa wa Singida kwa ushirikiano wanaotoa kwa serikali ili kuhakikisha mpango wa matokeo makubwa sasa unafikiwa.

MAHAFALI YA KUFUNGWA KWA MAFUNZO YA MGAMBO SINGIDA



Na.Edson Raymond
Kaimu mshauri wa mgambo wilaya ya Singida Ramadhan Njera ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida kujitokeza katika viwanja vya peoples kwa ajili ya kuishuhudia mahafali ya kufungwa kwa mafunzo ya mgambo tarafa ya unyakumi.

Njera ameyasema hayo leo wakati akizungumza na standard radio  ofisini kwake, ambapo amesema kuwa shughuli hiyo itaanza kesho kuanzia saa mbili na nusu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mlozi.

Amesema kuwa jumla ya wahitimu 90 wakiwemo wanawake 20 wanatarajiwa kupewa nishani zao na kula kiapo mbele ya mgeni rasimi Mwl. Mlozi

Aidha amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza ili kushuhudia shughuli nzima itakayo pambwa na burudani ya ngoma, gwaride la mwendo wa pole na haraka, maonyesho ya Singe na maonyesho ya kikundi cha kwata. 

Thursday, October 24, 2013

WAJAWAZITO WATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI




 Na.abdul bandola
Akina mama wajawazito wametakiwa kuwahi hosipitalini  ili kuepuka  mazingira yanayoweza kusababisha matatizo makubwa wakati wa kujifungua

Mratibu wa mradi wa JIDA unoshugulikia masuala ya wanawake na watoto Bi Amina Macona kutoka wilaya ya Igunga mkoani Tabora  amesema hayo katika semina iliyozishirikisha asasi zisizo za kiserikali katika ukumbi wa Kanisa la  kkkt la Msalaba mrefu mkoani Singida.
Amesema  kuwa iwapo watakuwa karibu na vituo vya kutolea huduma wataepuka vifo visivyo vya lazima kwa akina mama

Aidhsa amesema upatikanaji wa huduma kwa akina mama nihafifu kutokana na uelewa mdogo miongoni mwa akina mama nchini.
Kwa upande mwingine Bi Amina amesema kutokana na baadhi ya akina mama kuwa hatakama wanakadi za CHF na Imani potofu  husababisha baadhi ya wanawake kutofika katika vituo vya afya

DR.KONE KUKANUSHA ONGEZEKO LA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU SINGIDA




Na.edson raymond

Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone amekanusha taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kuwa mkoa wa Singida unakabiliwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

kutoa ufafanuzi huo kutokana na baadhi ya washiriki waliohudhuria katika kikao cha siku maalumu ya polisi kudai kwamba mkoa wa singida unakabiliwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Aidha amesema tangu mwaka 2008 mkoa wa singida umekuwa ukipambana na changamoto hiyo ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Amesema mafanikio ni makubwa kwani mkoa kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Outreach International umefanikiwa kujenga kituo cha Kids Center kinachotumika kuwapatia huduma muhimu watoto hao.

Dr Kone ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa singida kuwakamata watoto hao pindi wanapowaona na kuwafikisha katika kituo hicho, kwani kimejengwa kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kama vile elimu ya awali, na mahitaji mengine