Friday, October 18, 2013

WAZAZI TUPIGE VITA UMASKINI MARADHI NA UJINGA KWA WATOTO WETU





 Na.Emanuel gamasa
 Wazazi wametakiwa kufuata misingi ya baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere kwa kupiga vita umaskini,maradhi na ujinga kwa kuwahimiza watoto kuhudhuria  shule na kufuatilia maendeleo yao ya kitaaluma pindi wawapo shuleni

Kaimu mkuu wa magereza wa mkoa wa Singida Titus Mbuta amesema hayo katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Ititi iliyopo manispaa ya singida
Amesema iwapo wazazi watafuata misingi ya baba wa taifa kwa kupiga vita umaskini, maradhi na ujinga kwa kuhakikisha  watoto wao wanapata elimu ya kutosha na itakayo wanufaisha katika maisha yao
Kwa upande mwingine amewataka wazazi kuwa na ushikiano na walimu ili kuhakikisha watoto wao wanasoma kwa bidii na kutokomeza utoro


Thursday, October 17, 2013

HALMASHAURI ZATAKIWA KUCHUKUWA TAHADHARI YA MAGONJWA YA MILIPUKO

Na.Mwandishi wetu
Mamlaka  ya hali ya hewa Tanzania (TMA), imezitaka Halmashauri nchini pamoja na wizara ya afya,  kuchukua tahadhari ya milipuko ya magonjwa nyakati za mvua

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA , Ibrahim Nassib, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa warsha ya wadau mbalimbali wa mambo ya hali ya hewa na mazingira.

Amesema upo umuhimu kwa mamlaka hizo kujenga uhusiano na TMA pamoja na  kufuatilia mara kwa mara taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuchukua tahadhari hususani za milipuko ya magonjwa inayosabishwa  na ubovu wa miundombinu ya kupitisha maji msimu wa mvua.

Amesema milipuko mingi ya magonjwa wakati wa mvua imekuwa ikisababishwa na uchafu wa mitaro ambayo hushindwa kupitisha maji na hivyo kuzalisha wadudu wanaosababisha milipuko hiyo.

WATUMISHI WA SERIKALI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UWINDAJI HARAMU MKOANI MARA

Na.Mwandishi wetu
Zaidi ya watu 50 wakiwamo watumishi wa serikali wamekamatwa katika operesheni ya kitaifa ya kusaka wawindaji haramu na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.
Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na kikosi hicho katika mikoa ya Simiyu, Manyara, Mara na ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kesi za washitakiwa hao zimesajiliwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Safina Simufukwe na Hakimu wa Wilaya Mkuu, Hamadi Kasonso.
Ilielezwa kuwa washitakiwa hao kwa nyakati na maeneo tofauti walikamatwa na kikosi hicho wakiwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao wanashitakiwa kwa makosa ya kuingia katika hifadhini, kukutwa na nyara za serikali na kuendesha uwindaji haramu kinyume cha sheria

JUMLA YA TANI MILIONI 13.34 ZA CHAKULA ZIMEZALISHWA KWA MWAKA 2012/2013

Na.Beatrice Moses
Waziri wa nchi Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Steven Wasira  amesema jumla ya tani milioni 13.34 za chakula zimezalishwa kwa mwaka 2012/2013

Wasira amesema hayo jana wilayani Hanang Mkoani Manyara kwenye maadhimisho ya siku ya chakula duniani na kufafanua kuwa kiasi hicho kimetosheleza kwa asilimia 112

Amesema Serikali imejipanga kununua tani laki mbili za mazao ya nafaka baada ya kubaini kuwa wilaya 61 nchini zinakabiliwa na upungufu wa chakula

Naye kaimu mkuu wa mkoa wa manyara Bw. Khalid Mandia amesema mwaka huu mkoa huo umevuna zaidi ya tani laki tano za chakula