Tuesday, October 15, 2013

WATU ELFU MBILI WAKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

Na Imani Musigwa.
Watu elfu mbili wamekamatwa katika kipindi cha kuanzia  Januari hadi September mwaka huu wakituhumiwa kujihusisha na usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya
Takwimu hizo zimetolewa na  Rais Jakaya Kikwte wakati akihutubia katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru, wiki ya vijana na maadhimisho ya miaka 14  tangu afariki baba wa taifa hayati mwalimu Julius Nyerere
Amesema licha ya kukamatwa kwa watu hao pia dawa za aina mbalimbali zimekamatwa ikiwa ni pamoja na kilo 681 zaheloin
Aidha amezipongeza nchi ambazo zimekuwa msitari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya  na kuomba ushirikiano huo kuendelea kwa kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya vinahitaji mshikamano

WATANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO



Waziri wa usitawi wa jamii maendeleo ya vijana wanawake na watoto  
wa zanziber Zainabu  Omari Mohamed  amesema zipo jitihada za kutaka kuwagawa watanzania zinazofanywa na watu wasipenda umoja na mshikamano

Akitoa salaamu  wakati wa maadhimisho ya miaka 14 ya kifo cha baba wa taifa,kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na wiki ya vijana Bi Mohamed amesema hali hiyo ni hatari kwa msitakabili wa taifa na umoja wa watanzania

Amesema  endapo umoja wa watanzania unaonekana hivi sasa utatoweka, tanzania kusambaratika na kila mmoja atafedheheka na kuchekwa na dunia nzima

Amesema hayati baba wa taifa Mwl Julius Nyerere na Abed Aman Karume waliacha umoja ambao umekuwa mfano wa kuigwa duniani hivyo ili kuwaenzi hatunabudi  kuulinda,na  kuuendeleza mshikamano wa watanzania uliopo

Aidha amewataka watanzania  kutotoa nafasi kwa watu wanaopenda vyeo na madaraka yanayoashirika kuvuruga amani iliyojengeka kwa miaka mingi

BIDHAA ZAPANDA WAKATI WA SIKUKUU SINGIDA

Na.Anna Chiganga


Kupanda kwa bidhaa hasa za vyakula hasa kwa wakati huu wa kuelekea sikuu ya Eid el haji kunatokana na ugumu wa kupatikana kwa bidhaa hizo mkoani singida
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu mkoani singida wamesema hayo wakati wakizungumza na standard redio
Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyefahamika kwa jina la Khamisi Wadu  amesema kuwa wakazi wa singida na wanunuzi kwa ujumla hawanabudi kufahamu kuwa bidhaa zinapanda bei kutokana na kutopatikana kwa bidhaa hizo mkoani Singida
Ametaja baadhi ya vyakula ambavyo havizalishwi mkoani Singida kuwa ni pamoja na viazi mviringo (mbatata)
Ameshauri wakazi wa mkoa wa singida kuepuka dhana potofu kuwa  bidhaa zinapanda bei wakati wa sikuu bali kunatokana na ugumu wa kupatikana kwa bidhaa hizo

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA MKOANI SINGIDA


Na.Neema julius



Mtu mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi kifuani na mwingine kujeruhiwa mikono yote miwili baada ya watu wasiojulikana kuwavamia na kutaka kuwapora mali katika wilaya ya manyoni mkoani Singida
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Igwamadete kata ya iseke tarafa ya Nkonko wilayani manyoni baada ya mtu aliyejulikana kwa jina la Alody Joshua mwenye umri wa miaka 29 kupigwa risasi na majambazi hao
Aidha Daudi Azaliwa amejeruhiwa mikono yote miwili baada ya kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakitoka kwenye mnada wa Mpapa kuelekea nyumbani ndipo majambazi hao walipoanza kuwapiga na kuwanyanganya  fedha na kusababisha  kifo cha mtu huyo
Jeshi la polisi wilayani manyoni limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa watu watatu wanashilikiwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo na kwamba wanatarajiw akufikishwa mahakamani baada ya upelelzi kukamilika