Thursday, May 2, 2013

BONANZA LA STANDARD RADIO MEI MOSI 2013- MATUKIO KATIKA PICHA

Timu ya soka ya Standard Radio katika picha ya pamoja kabla ya mechi kati yao na mashabiki na wapenzi wa radio hiyo ijulikanayo kama STANDARD RADIO SALAAM CLUB FC muda mfupi kabla ya kuanza kwa mpambano ambao hata hivyo hakukuwa na mbabe baada ya timu zote kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja, mpambano huo ulichezwa katika uwanja wa ufukwe wa Ziwa Kindai mjini SIngida
 
 
Meneja wa Standard Radio Bw. Prosper Kwigize akisikilliza maelekezo ya kocha muda mfupi kabla ya mechi kuanza, Kwigize kutoka winga ya kulia ndiye aliyetoa pasi iliyosababisha kupatikana kwa bao la kusawazisha kipindi cha pili, mbele aliyeshika nyonga ni mchezaji centre half Imani Msigwa



























Kikosi cha Standard Radio FC kikijipanga kuzuia mpira wa adhabu kutoka kwa wapinzani wake STANDARD salaam club FC, Mwenye jezi namba 13 mgongoni ni mwanaspoti wetu Cales Katemana na jezi namba 12 ni Abdul Bandola  mtayarishaji msaidizi wa kipindi cha Michezo kinachorushwa na standard radio kila siku saa moja na nusu jioni



























Abdul Bandola (kulia menye bukta ya njano) star wa Standard Radio fc akichapa mwendo kufunga bao la ushindi, hata hivyo walinda mlango wa Salaam Club FC walifanikiwa kuzuia mashambulizi.

Meneja wa Standard Radio akiongoza kikosi cha mashabikii na watangazaji kuelekea uwanjani tayari kwa mtifuano wa Bonanza la Standard radio na Mei Mosi, Standard Radio Imeahidi kuendesha matamasha mbalimbali pamoja na mashindano ya soka kwa wanaume na wanawake kama sehemu ya kuitangaza Radio hiyo, Hivi karibuni lilifanyika tamasha kubwa na zuri wilayani Ikungi na inatarajiwa kufanyika tena mjini Singida na Iramba kabla ya kuenlekea Igunga na Nzega mkoani Taboba na baadaye matamasha hayo yatafanyika katika wilaya za Hanang na Mbulu mkoani Manyara

Bw. Boniface Mpagape (mwenye koti) ambaye ni Mhariri wa Standard Radio ambaye ni Mhariri akiongoza kikosi cha pili cha soka kutoka SR FM kuelekea uwanjani muda mfupi kabla ya mechi hiyo kuanza, Mpagape a.k.a Furgason) ndiye Kocha mchezaji wa timu ya soka ya Standard Radio

Wednesday, May 1, 2013

HELVETAS USWISS YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA STANDARD RADIO

Maafisa wa shirika la maendeleo la Uswiss wakizuru ofisi na jumba la matangazo la Standard Radio mkoani Singida katika ziara yao maalumu ya kutembelea kituoo hicho kwa malengo ya kuandaa mkakati wa kuanzisha ushirikiano katika kuandaa vipindi vya maendeleo hususani katika kilimo na ufugaji

katika kipicha kutoka kushoto Bw. Christian Bobst mpiga picha kutoka nchini Uswiss, Bi. Astrid Rana na Bi. Franca Palmy maafisa wa Helvetas wanaohusika na masuala ua ushirikiano na utunishaji wa mfuko wa maendeleo kwa ukanda wa Afrika na mwenye suti nyeusi ni Bw. Prosper Kwigize Meneja wa Standard Radio

katika picha ni Bw. Yusuph Salum mratibu wa shirika la Helvetas mkoanii Singida akiwa na Maafisa wake kutoka nchini Uswiss katika studio za Standard Radio, walikuwa wakishuhudia mafumo wa matangazo na namna matangazo yanavyorushwa na mtangazazji wa zamu

STANDARD WATOA FURSA YA MAFUNZO KWA VITENDO




























Kituo cha matangazo cha Standard Radio fm, kimepokea wanafunzi kutoka vyuoo mbalimali vya habari nchini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika kipindi cha May-July mwaka huu

 

Waliopokelewa ni wanafunzi kutoka vyuo vya Musoma Utalii, SAUT na Arusha Journalism ambao pamoja na mambo mengine watashiriki kazi za kihabari na utangazaji

 

Pichani ni baadhi ya wanachuo hao, ambao wamewasili leo Mei Mosi kuanza rasmi mafunzo yao

 

Kutoka kulia ni Bi. FATMA MUNA na MARIAM MATUNDU kutoka Arusha Journalism na Bw. MAZIKU MOTTO kutoka Musoma Utalii Tabora.



Friday, April 26, 2013

SHEREHE ZA MUUNGANO NA MAPAMBANO DHIDI YA NJAA SINGIDA


Source: SR/Chami

Ed: BM

Date: 26 April 2013.

 

SINGIDA

 

Wananchi mkoani Singida wametakiwa kudumisha amani, upendo na ushirikiano bila kusahau kuhifadhi chakula ili kujikinga na baa la njaa

Akihutubia katika siku ya maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar,  ambayo kiwilaya imefanyika katika kata ya mandewa viwanja vya mandewa, Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Qeen Mlozi amesema ni vyema wananchi kutumia maadhimisho hayo katika  kutekeleza shughuli za kiuchumi.

Amesema ili kutekeleza shughuli za kiuchumi lazima iwepo amani na utulivu na kwamba ni jukumu la kila mwananchi kuzuia uuzaji wa mazao ya vyakula yakiwa shambani, tena kwa bei ya chini ama kuuza kwa ujazo usio sahihi badala yake watumie ujazo uliowekwa kisheria.

Ameongeza kusema kuwa muungano huu utumike kama kiashiria kizuri cha amani na utulivu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwani kwa kufanya hivyo nchi itabadilika kimaendeleo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya sherehe za muungano ni amani,utulivu na maendeleo ni matokeo ya muungano wetu tuuenzi na kuulinda.