Friday, April 26, 2013

SHEREHE ZA MUUNGANO NA MAPAMBANO DHIDI YA NJAA SINGIDA


Source: SR/Chami

Ed: BM

Date: 26 April 2013.

 

SINGIDA

 

Wananchi mkoani Singida wametakiwa kudumisha amani, upendo na ushirikiano bila kusahau kuhifadhi chakula ili kujikinga na baa la njaa

Akihutubia katika siku ya maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar,  ambayo kiwilaya imefanyika katika kata ya mandewa viwanja vya mandewa, Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Qeen Mlozi amesema ni vyema wananchi kutumia maadhimisho hayo katika  kutekeleza shughuli za kiuchumi.

Amesema ili kutekeleza shughuli za kiuchumi lazima iwepo amani na utulivu na kwamba ni jukumu la kila mwananchi kuzuia uuzaji wa mazao ya vyakula yakiwa shambani, tena kwa bei ya chini ama kuuza kwa ujazo usio sahihi badala yake watumie ujazo uliowekwa kisheria.

Ameongeza kusema kuwa muungano huu utumike kama kiashiria kizuri cha amani na utulivu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwani kwa kufanya hivyo nchi itabadilika kimaendeleo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya sherehe za muungano ni amani,utulivu na maendeleo ni matokeo ya muungano wetu tuuenzi na kuulinda.

No comments: