Source:
SR/Monica
Ed:
BM
Date:
25 April 2013.
SINGIDA
Vijana wametakiwa kutojihusisha na matumizi ya
vidhibiti mimba pasipo kujua madhara yake.
Hayo yamesemwa na Bi Judith Kattani mratibu wa
Pro-life Tanzania jimbo la Singida na Kahama, alipokuwa akizungumza katika
kipindi cha Hoja ya leo jana kinachotangazwa na Standard Radio.
Amesema kuwa vijana wengi wanaathirika na madawa hayo
pasipo kujua kutokana na kukosa elimu ya kutosha.
Bi Judith amesema kutokana na matumizi hayo ya
vidhibiti mimba yanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maambukizi ya virusi
vya ukimwi kwa vijana kutokana na kuendekeza mapenzi na kujisahau katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Mratibu huyo wa Pro-life Tanzania Bi Judith Kattani
ametoa wito pia kwa wanafunzi kutojihusisha na vitendo vya mapenzi wakati wa
masomo, jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha
elimu kutokana na matumizi hayo ya vidhibiti mimba yanayowafanya kujiamini kuwa
hawawezi kupata mimba, jambo ambalo ni hatari kwao kwani huzuia mimba na
kusahau kuwa kuna gonjwa la ukimwi.
Aidha Bi Judith amewaasa wazazi kutoa ushirikiano kwa
walimu ili kushirikiana kwa pamoja kuweza kuwalea watoto ili kukuza maadili ya
vijana, kwani bila kufanya hivyo kiwango cha elimu kitazidi kushuka na
maambukizi ya virisi vya ukimwi yatazidi kuongezeka.
No comments:
Post a Comment