Friday, November 1, 2013

WAZIRI NAHODHA AONGOZA KUTOA HESHMA KWA MAREHEM LUTEN RAJAB MALIMA


Na.Iman Musigwa
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha jana amewaongoza maofisa wa JWTZ katika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Luteni Rajab Ahmed Mlima.

Luteni Mlima, aliuawa akiwa na wanagambo wa Kundi la waasi wa M23, katika Milima ya Gavana, karibu na Goma, chini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.

Viongozi wengine walioshiriki katika kutoa heshima zao za mwisho kwa ofisa huyo, ni pamoja na Mnadhimu mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba na viongozi mbalimbali wa Serikali

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa heshima hizo, Waziri Nahodha amesema taifa limepoteza mtu shujaa aliyekuwa akitetea roho za watu.

Amesema Serikali haitarudi nyuma katika masuala ya ulinzi wa amani, na kwamba itaendelea kutoa msaada wa ulinzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi hapo amani itakapopatikana.

UJANGIRI WATISHIA UHAI WA TEMBO NCHINI


Na.Imani Musigwa
Waziri wa  maliasili na utalii balozi khamis Kaghasheki ameliambia bunge  leo mjini Dodoma kuwa ujangiri unatishia uhai wa tembo nchini na kwamba tembo wako katika hatari ya kutoweka endapo hali hiyo haitadhibitiwa

 Kagasheki amesema hayo wakati akitoa tamko bungeni baada ya wabunge Khamisi Mkubwa na Kange Lugora kuomba bunge kuahilisha shuguli zake  ili kujadili ya masuala ya dharula na muhimu kwa taifa ambao ni mgogoro kati ya wafugaji na wakulima

Balozi Kagasheki amesema idadi ya tembo inashuka hali ambayo imeilazimu serikali kuanzisha oparation tokomeza ili kuokoa tembo wasipotee kabisa

 Spika wa bunge Anne Makinda alitoa fursa kwa waziri wa wizara husika  kujibu hoja  ambapo alianza waziri kagasheki na hatimaye waziri wa mifugo na uvuvu Bw mathayo Devid Mathayo

WAFANYAKAZI WAHUSISHWA NA WIZI WA SH.MILIONI 220


 
Na.Mwandishi wetu
Uchunguzi wa awali umeonyesha baadhi ya wafanyakazi walihusika katika tukio la uporaji wa Shilingi milioni 220, mali ya kampuni ya ujenzi ya Dott,

 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, amesema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo inayojenga barabara ya Same-Mkumbara kwa kiwango cha lami, wanadaiwa kuhusika na kuandaa njama za mpango wa uporaji wa fedha za mwajiri wao

Katika tukio hilo lililotokea mapema wiki hii watu wanaodaiwa kuwa  majambazi walivamia gari na kumteka Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Shuresh Bab ambaye  alikuwa akisafirisha fedha hizo bila ulinzi baada ya kuzitoa benki



Wakati uchunguzi huo wa awali wa polisi ukibaini hayo, bado  wakazi wa mji wa Moshi wanahoji zilipo  Shilingi milioni 140 kati ya milioni 220 zilizoporwa, licha ya polisi kusema wameokoa Shilingi milioni 80.



 

MADIWANI WAPINGA TOZO YA FAINI YA SH.LAKI TATU


Na.Edson Raymond
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamepinga sheria ndogo iliyopendekezwa na halmashauri hiyo ya kutoza faini shilingi laki tatu na kifungo cha miezi 12  jela kwa mzazi au mlezi atakayeshindwa kuchangia chakula shuleni.

 
Hatua hiyo imejiri jana katika baraza la madiwani la halmshauri ya wilaya ya Ikungi lililofanyika jana katika ukumbi wa halsmashauri manispaa ya Singida.

 
Mbuge wa Singida Mashariki Tundu Lisu kupitia (CHADEMA) amesema sheria itaibua mgogoro baina ya wananchi kwa kuwa hali ya chakula katika kaya za wilaya hiyo ni ngumu, hivyo akapendekeza sheria hiyo kufutwa.

 

Naye Mbunge Singida Magharibi Muhamed Misanga (CCM) hatua hiyo ni nzuri kwa kuwa inalenga wanafunzi kupata chakula shuleni lakini kunahaja ya kuangalia adhabu hiyo kwani licha ya kutaka kuwekwa kwa msisitizo wa upatikanaji wa chakula hicho, sheria hiyo itasababisha wananchi kuichukia serikali yao