Thursday, October 17, 2013

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA KWA WIZI WA MIFUGO

Na.Anna Chiganga

Mkazi wa  Mwasauya  mkoani Singida amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kubainika kutenda kosa wizi wa mifugo

Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo utemini Joyce Shilla amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Msunga Sima kuwa alitenda kosa hilo september 28 mwaka huu

Hakimu Shilla amesema mshitakiwa akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la rajabu sidadi waliiba mbuzi wawili na kisha kumchinja mmoja kabla ya mtuhumiwa rajabu kutoroka  na kukimbilia kusiko julikana

Mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na faini ya shilingi laki moja na elfu ishirini

Wednesday, October 16, 2013

RAIS JAKAYA AKUTANA NA VYAMA SITA VYA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM




 
Na.Mwandishi wetu

rais jakaya kikwete jana amekutanana na viongozi wa vyama sita vya siasa, vyenye uwakilishi bungeni, ikulu, jijini dar es salaam na kukubaliana mambo makuu mawili.

rais kikwete  amekubaliana na vyama vyote vya siasa vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013, kuyawasilisha haraka serikalini, ili kutafuta namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.

aidha amesema vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa katiba mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano, wa jinsi vitakavyosukuma mbele mchakato mabadiliko ya katiba ya nchi, kwa maslahi mapana ya nchi na mustakabali wa taifa.

katika makubaliano hayo, kituo cha demokrasia tanzania (tcd), kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.

FAMILIA YANUSURIKA KIFO BAADA YA KIMBUNGA KUEZUA NYUMBA MKOANI SINGIDA


Na.Hawa Mkhandi
familia moja imenusurika kufa kufuatia kimbunga kuezua nyumba wanamoishi ,katika wilaya ya ikungi mkoani singida

 
tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na nusu jioni, katika kijiji cha choda kata ya mkiwa tarafa ya ikungi

 
akizungumza na standard redio diawani wa kata ya mkiwa bw mathias sungita, ametaja walionusurika kuwa ni familia ya  bw saimon joram

 
imelezwa kuwa upepo mkali uliofuatana na kimbunga ulizingira nyumba ya bw sungita, na kuezua paa wakati familia hiyo ikiwa ndani

 
wananchi wametakiwa kutoa msaada kwa familia hiyo ambayo kwa sasa haina sehemu ya kuishi
 

WAISLAMU NCHINI WAMETAKIWA KUSHEREKEA KWA AMANI SIKUKUU YA EID


 
 
Na.Festo Sanga
 
waisilamu nchini wameungana na waislamu wengine nchini kusherehekea sikukuu a idd kubwa, ambapo pamoja na mambo mengine wametakiwa kuwajali watoto kwa kutoa sadaka kama mwenyezi mungu alivyowaamuru

 
wito huo umetolewa na msaidizi wa imamu bw ponda, hasa katika  swala ya eid  el haj, iliyofanyika katika msikiti wa kati new kiomboi  wilayani iramba

 
shekh ponda amesema iwapo waisilamu watawajali  na kuwathamini kwa kushiriki na watoto hao wakati wa sikukuu, watakuwa wametimiza ibada hiyo kama ilivyokusudiwa

 

aidha waumini wa dini ya kiisilami mjini kiomboi, wamewatakiwa kusherehekea eid el haj kwa amani na utulivu,  na kuepuka kufanya vitendo viouvu vinavyochukiza katika jamii