Tuesday, October 29, 2013

DIWANI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUVUNJA OFISI YA KIJIJI.

Na.Mwadishi wetu
Diwani wa
kata ya Iseke jimbo la Singida magharibi,Bw Emmanuel Jackson amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida  kwa tuhuma za  kuvunja ofisi ya kijiji cha Nkhoiree.

Mbele ya hakimu Asha Mwetindwa mwendesha mashitaka wa serikali,Petrida Muta,alidai tukio lilitokea  septemba 20 mwaka huu saa 8.30 mchana ambapo mshitakiwa alivunja nyumba kwa lengo la kuiba mali

Aidha katika shitaka la pili mtuhumiwa alidaiwa kuwa siku hiyo hiyo mshitakiwa baada ya kuvunja mlango wa nyumba inayotumiwa na serikali ya kijiji cha Nkhoiree,aliiba vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 298,000.

Vifaa vilivyoibwa ni pamoja , vitabu vya risiti ,hati za malipo, vitabu vya ushuru risiti za zahanati pamoja na  na madumu tupu

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na amerejeshwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena November 11 mwaka huu

OPARESHIN KIMBUNGA KUWEKA VIZUIZI BARABARANI.

Na.Imani Musigwa
Serikali imeiagiza mikoa jirani na ile inayofanya oparationi kimbunga kuweka  vizuizi vya barabarani ili kuimalisha doria na kufanya misako katika  nyumba za kulala wageni ili kuwabaini na kuwarudisha makwao wahamiaji haramu

Naibu waziri wa mambo ya ndani Bw Pereila  Silima amesema serikali imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na tatizo la wahamiaji haramu wasiotaka kurejea makwao ama wanaorejea kwa siri
Wakati huo huo serikali imesema itachunguza na kuchukua hatua stahiki  kwa watendaji waliohusika katika kuwaondoa wahamiaji kinyume na  haki za binadamu katika zoezi la operation kimbunga linaloendelea
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa shamsi Vuai Nahodha  amesema hayo wakati akijibu  swali la mkuu wa kambi ya upinzani bungeni mjini Dodoma Bw Freeman Mbowe  aliyetaka kujua serikali itachukua hatua gani endapo itagundulika kuwepo kwa uvunjifu wa haki za biandamu katika zoezi hilo

UMUHIMU WA KUCHANGIA UJENZI WA VYUMBA VYA MAABARA SHULENI

Na.Neema Mwampamba
Mkuu wa mkoa wa singida Dr Perseko Korne amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa serikali ili kufanikisha ujenzi wa maabara katika shule za sekondari
Akizugumza na standard radio ofisini kwake Dr Korne amesema ni lazima kila mzazi kuwajibika kwa kutoa mchango wa ujenzi wa maabara ili kuwawezesha wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kujengewa msingi mzuri
Aidha amesema juhudi zinafanyika ili kuhakikisha maabara za masomo ya Biology Chemia na phizikia zinakamilika katika shule zote ifikapo February 2014
Hata hivyo amewapongeza wakazi wa mkoa wa Singida kwa ushirikiano wanaotoa kwa serikali ili kuhakikisha mpango wa matokeo makubwa sasa unafikiwa.

MAHAFALI YA KUFUNGWA KWA MAFUNZO YA MGAMBO SINGIDA



Na.Edson Raymond
Kaimu mshauri wa mgambo wilaya ya Singida Ramadhan Njera ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida kujitokeza katika viwanja vya peoples kwa ajili ya kuishuhudia mahafali ya kufungwa kwa mafunzo ya mgambo tarafa ya unyakumi.

Njera ameyasema hayo leo wakati akizungumza na standard radio  ofisini kwake, ambapo amesema kuwa shughuli hiyo itaanza kesho kuanzia saa mbili na nusu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mlozi.

Amesema kuwa jumla ya wahitimu 90 wakiwemo wanawake 20 wanatarajiwa kupewa nishani zao na kula kiapo mbele ya mgeni rasimi Mwl. Mlozi

Aidha amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza ili kushuhudia shughuli nzima itakayo pambwa na burudani ya ngoma, gwaride la mwendo wa pole na haraka, maonyesho ya Singe na maonyesho ya kikundi cha kwata. 

Thursday, October 24, 2013

WAJAWAZITO WATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI




 Na.abdul bandola
Akina mama wajawazito wametakiwa kuwahi hosipitalini  ili kuepuka  mazingira yanayoweza kusababisha matatizo makubwa wakati wa kujifungua

Mratibu wa mradi wa JIDA unoshugulikia masuala ya wanawake na watoto Bi Amina Macona kutoka wilaya ya Igunga mkoani Tabora  amesema hayo katika semina iliyozishirikisha asasi zisizo za kiserikali katika ukumbi wa Kanisa la  kkkt la Msalaba mrefu mkoani Singida.
Amesema  kuwa iwapo watakuwa karibu na vituo vya kutolea huduma wataepuka vifo visivyo vya lazima kwa akina mama

Aidhsa amesema upatikanaji wa huduma kwa akina mama nihafifu kutokana na uelewa mdogo miongoni mwa akina mama nchini.
Kwa upande mwingine Bi Amina amesema kutokana na baadhi ya akina mama kuwa hatakama wanakadi za CHF na Imani potofu  husababisha baadhi ya wanawake kutofika katika vituo vya afya

DR.KONE KUKANUSHA ONGEZEKO LA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU SINGIDA




Na.edson raymond

Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone amekanusha taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kuwa mkoa wa Singida unakabiliwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

kutoa ufafanuzi huo kutokana na baadhi ya washiriki waliohudhuria katika kikao cha siku maalumu ya polisi kudai kwamba mkoa wa singida unakabiliwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Aidha amesema tangu mwaka 2008 mkoa wa singida umekuwa ukipambana na changamoto hiyo ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Amesema mafanikio ni makubwa kwani mkoa kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Outreach International umefanikiwa kujenga kituo cha Kids Center kinachotumika kuwapatia huduma muhimu watoto hao.

Dr Kone ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa singida kuwakamata watoto hao pindi wanapowaona na kuwafikisha katika kituo hicho, kwani kimejengwa kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kama vile elimu ya awali, na mahitaji mengine

WANAFUNZI WAWILI WA KIDATO CHA NNE KUBAINIKA NA UJAUZITO







Na.Mwandishi wetu
 Bodi ya Shule ya sekondari ya Ibaga wilayani Mkalama imewafukuza shule wanafunzi wawili wa kike,kati ya wanafunzi 77 wa kidato cha nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wa taifa mwezi ujao baada ya kubainika kuwa na ujauzito.

Mkuu wa shule ya sekondari Ibaga,Bw Wilsoni Mchemba amesema hayo kwenye taarifa aliyotoa kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya nne ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo

Amesema shule kutokuwa na mabweni, wanafunzi  kutembea zaidi ya kilomita tano ni moja ya sababu zinazosababisha  matatizo hayo ikiwa ni pamoja na  kupata ujauzito

Aidha Bw Mchemba amewataka wazazi kushirikiana na uo

UZEMBE KWA BAADHI YA VIONGOZI HUCHANGIA KUZOROTESHA MAENDELEO



Na.Neema julius
 Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi Fatuma Hasan Toufiq amesema chanzo cha kuzorota kwa maendeleo vijijini ni kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya viongozi na kusababisha ushirikiano duni kati ya wananchi na viongozi hao

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa tarafa ya kilimatinde wilayani manyoni Bi Fatuma amesema kuwa ushirikiano duni kati ya viongizi maeneo ya vijijini ni kutokana na ushirikishwaji duni wa shuguli zenye tija kwa jamii na kusababisha miradi ya maendeleo kutofika kwa wakati katika vijiji vya wilaya ya manyoni

Aidha Bi Toufiq ameitaka idara ya ujenzi wilayani hapo kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa wilayani kabla ya mingine kuanza kutekelezwa kutokana na baadhi ya majengo kutokuwa na viwango jambo ambalo linasababishwa na  idara hiyo kwa kuendeleza uzembe na kusahau kutembelea maeneo ya vijijini

Kwa upande mwingine amewataka viongozi wa idara hiyo kujirekebisha ili majengo yaweze kukidhi viwango kulingana na maelekezo ya serikali