Source;
SR/ Neema J
Ed;
Date;
March, 27, 2013
SINGIDA
Mkuu
wa wilaya ya singida Bi Queen Mlozi, amelita jeshi la polisi kutumia mafunzo watayoyapata ipasavyo,
na kusema yatawasaidia kuongeza maarifa mapya na kuleta
mabadiliko, kwa kuwajibika katika utendaji kazi wao.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mafunzo ya jeshi polisi kazini jana Bi Mlozi amesema,
maendeleo hayawezi kuja bila changamoto, hivyo kuwataka polisi kuhamasishana
katika utendaji kazi wao, bila
kukata tamaa kwani elimu haina mwisho.
Kwa
upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa, amesema lengo
la mafunzo hayo kutawezesha afisa
askari na polisi ufanisi wa kufanya kazi, kuleta mabadiliko katika utendaji kazi wao,
pamoja na kuliwezesha jeshi la polisi kufanya kazi kwa ufanisi, usasa, uweledi
pamoja kushirikishaisha jamii, juu ya ulinzi wa mali zao.
Naye
mkufunzi wa elimu ya watu wazima mkoa
wa singida Bw Musa Nkungu, ambaye ni
mmoja kati ya watoa mafunzo
kwa jeshi la polisi, amesema mafunzo hayo yatawasaidia polisi kupata
mafaniko, ikiwa ni pamoja na muhitimu
kutunikiwa cheti atakapo hitimu
mafunzo kazini, na kupandishwa
cheo na kuongezewa madaraka ya uongozi, katika jeshi la polisi hivyo kuwataka polisi kuhudhuria katika
mafunzo, ili waongeze ufanisi wa kazi .
Source;
Tanzania Daima
Ed;
Date;
March, 27, 2013
DAR ES SALAAM
Serikali imesema haitamvumilia mtu atakayeendesha shughuli za
kibinadamu, katika maeneo tengefu lengo
ni kunusuru ikolojia ya Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Loliondo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri
wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema wananchi walioingia
ndani ya pori tengefu la Loliondo, wanatakiwa kuondoka mara moja.
Balozi Khagasheki amesema kutokana na mgogoro ulioko Loliondo
kwa muda mrefu sasa, serikali imepata ufumbuzi ambapo wananchi wanatakiwa kutii
sheria bila kushurutishwa.
Aidha amesema ili, kutatua migogoro iliyopo serikali itatenga
na kuchukua sehemu ya ardhi ya Pori Tengefu la Loliondo, yenye ukubwa wa
kilomita za mraba 1500 kutoka kwenye eneo la kilomita za mraba 4000, za pori
hilo.
Source;
SR/ Elizabeth, Martine
Ed;
Date;
March, 27, 2013
SINGIDA
Wanachama
wa chama cha walemavu wasiioona mkoani Singida TLB, wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali katika maisha yao ya kila siku, na kusababisha kushindwa
kutekekeleza majukumu yao.
Akizungumza
na standard radio mwenyekiti wa chama cha walemavu wa kutoona mkoani singida
Bw. Hassani kingugu , ambaye pia ni mlemavu wa kutoona amesema kuwa, changamoto
zimekuwa ni tatizo katika maisha yao jambo linalopelekea wao kushindwa kumudu
maisha, na kubaki wanahangaika.
Bw.
Kingugu amezitaja changamoto hizo kuwa ni jamii kuwa na mtazamo hasi kwa kudhani
walemavu hawawezi kitu, uhaba wa shule, vifaa vya kujifunzia na kufundishia,
kubadilika kwa mitaala, kutoshirikishwa kwenye shughuli za ujasiriamali, pamoja
na viongozi mbalimbali kutowaelimisha wanajamii, namna ya kuwajali na
kuwahudumia walemavu wasioona.
Aidha
ametoa wito kwa jamii kutowabagua walemavu na badala yake itambue mchango wao
katika maisha ya kila siku, kwani kuna walimu ,wafanyabiashara, mahakimu ambao
ni walemavu.
Source;
Tanzania Daima
Ed;
Date;
March, 27, 2013
TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Galawa, amesema
tatizo la vijana wengi kukosa ajira linaweza kumalizika ikiwa watavitumia vyuo
vya ufundi stadi (VETA), vilivyopo katika maeneo yao.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya
kutembelea chuo cha Veta cha jijini Tanga, kwa lengo la kujua hatma ya vijana
hao, kupatiwa nafasi mbalimbali, ili hatimaye waondokane na tabia ya
kurandaranda mitaani.
Galawa ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kutambua fursa
hiyo, akiwahakikishia kwamba wanaweza kujikwamua na suala la umaskini,
linalowakabili vijana wengi, kutokana na kukosa shughuli za kufanya.
Naye
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi Veta Tanga, Alphonce Kibasha, amemwambia mkuu wa
mkoa kwamba changamoto inayowakabili ni uhaba wa majengo, ya kuweza kuchukua
vijana wengi kwa wakati mmoja.