Tuesday, July 3, 2012

WAMASAI ENGI KARET WAAMUA KUSOMESHA WATOTO

Sirika la kimisioni la ROHO MTAKATIFU la kanisa Katoliki limejikita katika vijiji ambavyo ni makazi wa WAMASAI huko mkoani Arusha katika wilaya ya LONGIDO ambapo kupitia katika shule ya sekondari SUMA Egi Karet zaidi ya watoto 100 wa kabila la wamasai wanapatiwa elimu

Hata hivyo zipo changamoto nyingi sana za kimiila na utamaduni wa wamasai kutopenda kuwasomesha watoto wao ili wabaki kuwa wachungaji wa mifugo kwa watoto wa kiume na watoto wa kike waolewe ili kuongeza idadi ya mifugo
Pongezi za pekee ziwaendee mapadre wa Roho mtakatifu EGI KARET LONGIDO, Padre Karumuna na Padre Chundu waliompokea mkurugenzi wa Standard Radio aliyetembelea kijiji cha Eng karet na kushuhudia watoto wa kimasai wakisoma

watoto wote walitamani kuwa wanahabari mara tu waliporekodiwa na kufundisha juu ya mfumo wa utayarishaji wa habari na vipindi vya radio, Sina shaka Padre Karumuna atawawezesha siku moja waitembelee Standard Radio mjini Singida kwa ajili ya ziara ya mafunzo, kwa njia hii tutaibua vipaji vingi kwa watoto walioko sekondari.

"DAFTARI ULILONALO DAWATINI NA UBAO WA KUANDIKIA DARASANI NDIYO NJIA YA MAISHA YAKO MWANAFUNZI"

No comments: