MKUU WA MKOA SINGIDA APONGEZA APONGEZA UJIO WA STANDARD RADIO
Mkuu wa mkoa wa Singida amepongeza uamzi wa kampuni ya Standard Voice LTD wa kuja kuwekeza katika mawasiliano mkoani Singida hasa kwa kuanzaisha kituo cha radio ya Standard Radio FM na kukiri kuwa ni mapinduzi ya maendeleo kwa mkoa.
Akiongea na meneja wa Standard Radio fm Ndg Prosper Kwigize jana mjini Singida wakati wa semina ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania TRCA, mkuu hyo wa mkoa Dr. Paseko Kone amekiri kuwa uanzishwaji wa Radio itakayorusha matangazo yake kutoka Singida ndio njia pekee ya kuinua uchumi wa wananchi pamoja na kupanua wigo wa mawasiliano.
Aidha katika maelezo yake mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone amepongeza vyombo vya mawasiliano nchini kwa kuwawezesha wakulima mkoani humo kupata masoko ya mazao kwa njia rahisi na hivyo kukuza uchumi wa kaya zao
Dr. Kone amebainisha hayo jana (jumanne) mkoani Singida wakati akifungua warsha ya wadau wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA iliyokuwa ikijadili ukuaji wa sekta ya mawasilano Tanzania
Alibainisha kuwa, katika kipindi kifupi cha ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano husani uwepo wa simu vijijini, matangazo ya Radio na Runinga, wakulima wameweza kujua wapi kuna soko la mazao yao
“kila ninapokwenda vijijini wananchi hususani wakulima wa vitunguu wananiambia wazi kuwa sasa soko la vitunguu liko wazi na hawahangaiki sana kuvisafirisha kwenda sokoni balii wateja kuwafuata wenyewe, na hata wanaposafirisha wanakwenda wakijua bei hivyo hawawezi kuibiwa au kuuza kwa hasara” alisema Dr. Kone
Hata hivyo pamoja na pongezi hizo, mkuu huyo wa mkoa wa Singida ameonya kuwepo kwa matumizi mabaya ya mawasiliano ambayo yamekuwa yakipotosha jamii na kupoteza utamaduni na maadili ya jamii
Alieleza kuwa, matangazo mengi hasa katika vyombo vya matangazo hayazingatii maadili na hivyo huchochea kuporomoka kwa maadili na kupoteza uzalendo miongoni mwa watanzania
“Mimi ninashangaa, unaweza ukaona kipindi katika Runinga kikionesha mambo ambayo kwa hakika ni potofu kabila, ni kinyume cha maadili ya mtanzania, sasa najiuliza ni nani anaruhusu matangazo au vipindi hivyo kuoneshwa au kutangazwa? Taifa letu wanataka lielekee wapi jamani” alieleza Kone kwa masikitiko makubwa.
Wakati huo huo, mkuu huo wa mkoa wa Singida ametumia fursa hiyo kutoa onyo kwa watu ambao wameanza kupotosha dhana nzima ya sensa ya watu na makazi na kueleza kuwa makampuni ya mawasiliano zikiwemo radio na runinga zitumie vyombo vyao kuhamasisha jamii kujitokeza kuhesabiwa
Dr. kone amebainisha kuwa yapo makundi ya watu ambayo yanaeneza uvumi kuwa serikali anataka kuwahesabu watu ili kupandisha kodii na kuanzisha kodi mpya hasa za mifugo na kwamba hayo ni maneno ya kupotosha jamii
Warsha ya wadau wa mawasiliano iliandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TRCRA kwa lengo la kuwawesha wadau kutambua wajibu na haki ya matumizi ya vyombo vya mawasiliano kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Mwisho