Source:
SR/Chami
Ed:
BM
Date:
26 April 2013.
SINGIDA
Wananchi
mkoani Singida wametakiwa kudumisha amani, upendo na ushirikiano bila kusahau
kuhifadhi chakula ili kujikinga na baa la njaa
Akihutubia
katika siku ya maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambayo kiwilaya imefanyika katika kata ya
mandewa viwanja vya mandewa, Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Qeen Mlozi
amesema ni vyema wananchi kutumia maadhimisho hayo katika kutekeleza shughuli za kiuchumi.
Amesema
ili kutekeleza shughuli za kiuchumi lazima iwepo amani na utulivu na kwamba ni
jukumu la kila mwananchi kuzuia uuzaji wa mazao ya vyakula yakiwa shambani,
tena kwa bei ya chini ama kuuza kwa ujazo usio sahihi badala yake watumie ujazo
uliowekwa kisheria.
Ameongeza
kusema kuwa muungano huu utumike kama kiashiria kizuri cha amani na utulivu
katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwani kwa kufanya hivyo nchi
itabadilika kimaendeleo.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya sherehe za muungano ni amani,utulivu na
maendeleo ni matokeo ya muungano wetu tuuenzi na kuulinda.