pichani ni viongozi wa serikali ya wilaya ya Iramba pamoja na Meneja wa Standard Radio fm, Bw. Prosper Kwigize (katikati mwenye Kaunda suti) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tamasha la kuitangaza Radio hiyo wilayani Iramba
Wakazi
wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, wametakiwa kuitumia Standard Radio katika
kufikisha ujumbe kwa jamii na kushiriki kikamilifu katika uandaaji wa vipindi
vya kuelimisha umma.
Wito
huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahaya Nawanda, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu tawala wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya
Naniya, wakati wa utambuilisho wa Standard radio kwa wakazi wa wilaya hiyo
uliofanyika katika stendi ya mabasi ya mjini Kiomboi.
Katibu tawala wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Nania (mwenye suti na miwani) akijiandaa kutoa hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Nawanda)
Amesema
mawasiliano ni kitu muhimu katika jamii kwani hurahisisha mambo mengi ikiwa ni
pamoja na kufikisha ujumbe kwa haraka, lamoja na kuweza kujipatias wateja wengi
kutokana na kujitangaza kibiashara.
Awali
meneja wa Standard radio Bw. Prosper Kwigize amesema, Standard radio ipo ili
kukidhi haja ya wakazi wa mkoa wa Singida kwani ni radio ya kwanza kuanza
kutangaza ndani ya mkioa wa Singida tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika
zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
Bw. Kwigize amesema msimamo wa Standard radio
haugemei upande wowote kidini, kisiasa au kijamii, bali ni radio ambayo inatoa
huduma zake kwa wananchi wote bila ubaguzi, na kuwataka wakazi wa wilaya ya
Iramba kuitumia ipasavyo.
No comments:
Post a Comment