Wednesday, June 5, 2013
WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KWA USTAWI WA JAMII
pichani ni viongozi wa serikali ya wilaya ya Iramba pamoja na Meneja wa Standard Radio fm, Bw. Prosper Kwigize (katikati mwenye Kaunda suti) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tamasha la kuitangaza Radio hiyo wilayani Iramba
Wakazi
wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, wametakiwa kuitumia Standard Radio katika
kufikisha ujumbe kwa jamii na kushiriki kikamilifu katika uandaaji wa vipindi
vya kuelimisha umma.
Wito
huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahaya Nawanda, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu tawala wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya
Naniya, wakati wa utambuilisho wa Standard radio kwa wakazi wa wilaya hiyo
uliofanyika katika stendi ya mabasi ya mjini Kiomboi.
Katibu tawala wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Nania (mwenye suti na miwani) akijiandaa kutoa hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Nawanda)
Amesema
mawasiliano ni kitu muhimu katika jamii kwani hurahisisha mambo mengi ikiwa ni
pamoja na kufikisha ujumbe kwa haraka, lamoja na kuweza kujipatias wateja wengi
kutokana na kujitangaza kibiashara.
Awali
meneja wa Standard radio Bw. Prosper Kwigize amesema, Standard radio ipo ili
kukidhi haja ya wakazi wa mkoa wa Singida kwani ni radio ya kwanza kuanza
kutangaza ndani ya mkioa wa Singida tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika
zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
Bw. Kwigize amesema msimamo wa Standard radio
haugemei upande wowote kidini, kisiasa au kijamii, bali ni radio ambayo inatoa
huduma zake kwa wananchi wote bila ubaguzi, na kuwataka wakazi wa wilaya ya
Iramba kuitumia ipasavyo.
MTOTO MCHANGA ATELEKEZWA NA MAMAE MJINI SINGIDA
Mtoto anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita ameokotwa akiwa ametupwa katika kitongoji cha unyakumi kata ya mandewa mkoani Singida
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji hichi bi.Hadija Msumari amesema
mtoto huyo wa jinsia ya kiume ameokotwa
katika nyumba iliyokuwa ikijengwa ya
bwana Sadiki juma.
Amesema
baadhi ya vitu alivyokutwa navyo ni pamoja na begi dogo la nguo,chupa ya uji,na
kadi ya kliniki
Akifafanua zaidi amesema kadi ya mtoto inaonesha kwa mara ya mwisho alipelekwa katika kliniki ya uhasibu mjini singida na anaishi kitongoji cha misake na mwenyekiti wa eneo hilo ni bwana Hamisi Mdadi huku jina la mtoto na wazazi likiwa limefutwa
Aidha
mmoja wa mashuhuda ambae amemuokota mtoto huyo bi.Hadija shabani amesema alikuwa akipita jirani na
eneo la tukio majira ya saa mbili asubuhi na kumsikia mtoto akilia kwa muda
mrefu ndipo bila kuhisi dalili yoyote ya msaada
ndipo alipoamua kuingia ndani na kumkuta mtoto akiwa peke yake
Jeshi
la polisi mkoani singida limemchukua mtoto huyo kufanya uchunguzi ili kumbaini
anaehusika na tukio hilo la kinyama
Imeandikwa na Edilitruda Chami
Subscribe to:
Posts (Atom)