Friday, September 28, 2012

JOTO LA UCHAGUZI LAPANDA - CCM IRAMBA

Na.   Phesthow   Sanga
Iramba, Singida

Chama Cha Mapinduzi {CCM} Wilaya  ya  Iramba  Mkoani  Singida,Kinajiandaa  Kufanya  Uchaguzi  wake  Mkuu  wa  ngazi  ya  Wilaya  septemba 30- Mwaka huu  kwa  Nafasi  ya Mwenyekiti  wa Wilaya, pamoja  na  Nafasi ya  {NEC}Taifa.
Katibu  wa  Wilaya  ya  Iramba  Mathias  Shidagisha  amewataja  wagombea  kwa  Nafasi  ya Mwenyekiti   wa  Wilaya Ambao  majina  yao Yamerudishwa  kutoka  Halmashauri  kuu  ya  ccm Taifa, ni  pamoja  na  Charles  Mkumbo Makala ,Moses  Nalogwa  Kitonka ,na  Mwenyekiti  ambaye   muda  wake Unaisha  Wilson Nico Msengi .
Shidagisha  amewataja  Wagombea  Wengine   Wa nafasi  ya  Halmashauri kuu  ya  ccm Taifa {NEC} Kuwa  ni   Joseph  Gerson  Mlewa ,Michael Shankolo Kitundu,  na  Aliyekuwa  Mbunge wa  jimbo la  Iramba Magharibi  Juma Hassan Killimbah.
Aidha   Katibu huyo  wa  ccm  Iramba  Ameeleza  kuwa   Nafasi  zingine  6  zinazo tarajiwa  kufanyiwa  Uchaguzi  ni  pamoja  na Katibu Siasa na Uenezi Wilaya  Nyenye  Wagombea  Watatu  kati ya  hao ni  Daudi Amos Madelu ,Wazaeli Nahuva Maja,na Moses Nalogwa  Kitonka.
Nafasi  nyingine  ni  ya  Katibu Uchumi  na  Fedha  Wilaya  nayo yenye  Wagombea  watatu  Ambao ni Charles  Mkumbo  Makala ,Jen  Henry  Mtata, pamoja  na  Zacharia Elias Mkoma  .
Aliwataja  Wajumbe  wengine  wanaogombea  Ujumbe  wa  Mkutano  Mkuu  wa  Taifa  ni  pamoja  na  Mkuu wa Wilaya  ya I ramba  Yahya  Nawanda ,Nafasi  Inayogombaniwa  na wagombea  wapatao  14.
Nafasi  nyingine  ni Wajumbe  wa Halmashauri kuu  ya Wilaya  Ambayo  Lina  kundi  la Wanawake  lenye  Wagombea  Wawili  kundi  Lingine  ni la Wazazi   Wagombea  Watano  na kundi  Jingine  ni la Vijana  Lenye Wagombea Watano pia .
Mathias  Aliwataja  Wajumbe Wengine  Watano   wanaogombea  Ujumbe  wa  Mkutano  Mkuu wa  Mkoa  ni  Marimu  Zabron  Rajabu,  Juma Swalehe Mhampa,  Humphrey Timotheo Shango, Chanima Hamud  Seifu,pamoja  na   Mathayo  Shango  Nguli.
Aidha  wajumbe  Wengine  wa Halmashauri  kuu ya Mkoa  toka  Iramba  ni Rehema Mssa  Mkasa ,Kinota Omary Khamis  {JB},Timothy  Wilson  Lyanga,Jane  Henry  Matata,  Elimamba Msafiri Lula, na  SaidRamadhani Tyunu .
Aidha Katibu wa Wilaya  Mathias,  Amewaeleza  Wagombea  Pamoja na  Wapiga  kura  kujihadhari  na  Tabia  ya  kutoa na kupokea  Rushwa  kwani wao  Wameandaa  VYombo  vyote  vya Usalama  kupambana  na  Changamoto  hiyo  kwa kila  Mtu  atakaye  jihusisha  na Mtandao huo.
Hivyo Mtu yeyote asije   kuulalamikia  Uongozi  kama  Atapatikana  na tatizo  hilo  la kutoa na kupokea  Rushwa ,na Amewaomba  Wajumbe  wote ambao  ni Wapiga  Kura  siku  hiyo  ya tarehe 30  kujitokeza  kwa  Wingi  ili Waweze  kumliza  kazi hiyo  iliyobakia  ya kupata  Viongozi  wa Ngazi ya Wilaya.
                                                       MWISHO.

Thursday, September 27, 2012

MAHAKAMA YAPIGA STOP UCHIMBAJI WA MADINI

NA  Phesthow  Sanga .  Iramba  
Mahakama  Wilayani  Iramba  Mkoani  wa  Singida,Imepiga  marufuku  shughuli  za  Uchimbaji  wa Madini  Ya  dhahabu  katika  Machimbo  ya  Sekenke wilayani  humo  kutokana  na Eneo  hilo kuwa na Mgogoro  Mkubwa   Ambao  Umeshindikana  kusuluhishwa na mkuu wa wilaya  Yahya Nawanda .
Amuri  hiyo  halali Imetolewa  jana  na Hakimu mkuu  Mfawidhi  wa Mahakama hiyo  Mrisho  K.Mrisho Baada  ya kusikiliza  kesi na, 10 ya mwaka 2012 iliyokuwa  inahusu  Zuio la Uchimbaji  Madini,  kati ya Mlalamikaji  John Binner  na   Emmanuel  Magai.
Kwa   Mujibu  wa  hukumu  iliyosomwa  na hakimu huyo  Ilieleza  kuwa, Awali Emmanuel  Magai alipeleka  Ombi  Mahakamani  hapo kuomba  Mahakama  Imzuie John Binner  kujihusisha  na kutaka asilimia 20 ya mapato  ya madini  yanayopatikana  mgodini hapo.
Aidha  ilielezwa  kuwa ,John Binner  naye  alipeleka  Maombi  Mahakamani  hapo  kumzuia  Emmanuel Magai  Kutoendelea  na  Uchimbaji  kwa  Sababu  ameshindwa  kumlipa  Binner  asilimia 20 mwenye  Leseni  halali na mmiliki  wa Mgodi  huo.
Hakimu  Mrisho  alitupilia  mbali Ombi  la Emmanuel  Magai  ,kwa kile alichodai kuwa lilikuwa na Mapungufu ,Alisema  kwa upande wa  John  Binner   vilele kulikuwa  na mapungufu kadhaa  hivyo Mahkama  Inatoa  Amri  ya Mtu yeyote  kutojihusisha  na  Uchimbaji  kuanzia  tarehe  ya kusomwa hukumu  hiyo  jana.
Hakimu huyo  Alisema kuwa,  kwa  kuwa ,Kesi  mama  Inaendelea  katika  Mahakama hiyo,hivyo wote  watulie  Mpaka Mahakama  Itakapotoa  Maamuzi  kuwa  mwenye Uhalali  wa Eneo  hilo ni nani; na hili  Zuio ni la muda  tu.
Kwa  upande wake  Emmanuel  Magai, alisema  kuwa  Yeye ameridhika  na Uamuzi  wa Mahakama kwani  Eneo lililotajwa  ni la kijiji Cha  Mgongo na si Eneo la kijiji Cha   Nkonkilangi   anako fanya kazi yeye.
        Aidha kwa Upande wake  John Binner  naye alisema kuwa ,yeye  ameona   Mahakama  Imetenda  haki iliyopaswa kuitenda  kwa kuwa Tangu amiliki Eneo hilo kihalali  hajawahi  kulipwa  hata shilingi moja na Emmanuel , kama  Walivyokubaliana.

UJUMBE WA DHARULA

STANDARD VOICE LIMITED

STANDARD RADIO FM, P.O BOX 62, SINGIDA TANZANIA,
+255 787592056, +255 786 200518, +255 764 243377srfm2011@gmail.com, standardradio2011@hotmail.com, http//www.standardradiofm.blogspot.com

September 27, 2012

Kwa Watangazaji wateule

Doris Meghji, Eufrazia Mathias, Editruda Chami, Edson Raymund, Veronica Medard na Abdul Bandola

YAH: UJUMBE WA DHARULA

Ninatumaini mnaendelea vema na maandalizi ya maisha mapya ya kazi na Standard Radio FM baada ya kuteuliwa kuwa watumishi wapya kufuatia kufaulu usaili uliofanyika Septemba 17 mwaka huu; Ninachukua fursa hii kukutakia maandalizi mema.

Hata hivyo kutokana na kuchelewa kupatikana kwa barua toka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ambayo tuliitrajia kutufikia kabla ya septemba 26 ikituruhusu kuanza rasimi vipindi (Radio Productions), tunalazimika kuahirisha tarehe ya kuripoti kazini kutoka Octoba Mosi hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Sina shaka huu ni usumbufu kwenu kwani hamkutarajia kupata ujumbe huu wa dharula, Tunaomba Radhi kwani jambo hili liko nje ya uwezo wetu na si busara kuwaruhusu kuja kuripoti kazini wakati hakutakuwepo na shughuli za uzalishaji wa vipindi na matangazo mengine.

Tunasisitiza uvumilivu kwa kipindi hicho cha mwezi mmoja tu yaani siku 30 pekee za kukupa fursa ya kuendelea kujiandaa kuja kuchapa kazi hapa Standard Radio Fm 90.1 Mhz Singida.

Narudia kuomba radhi kwa usumbufu huu.

Wako katika tasnia


Prosper L.N Kwigze
Meneja Mradi
Standard Radio FM

Sunday, September 23, 2012

JIKWAMUE KIUCHUMI - MAKALA KUTOKA ARUSHA

 
Na:
Matinde  Nestory
Katika hali ya kawaida ujasiri ni ile hali ya uthubutu wa kuamua kuanzisha biashara, na ujasiri huo utakuletea faida katika biashara yako, na mali ni ile hali ya kuwa na uwezo wa kumiliki kitu mfano fedha,mifugo,bidhaa  pamoja na hayo naweza sema kuwa ujasiriamali ni ile hali ya kujiajiri mwenyewe bila ya kuwa na mkataba na mtu.
Nia ya kuandika makala hii ni kutaka mwananchi kujifunza ujasiriamali ambao utakupanua kimawazo,kimtazamo na hata kiakili,pamoja na hayo ujasiriamali utakusaidia kujua mbinu mbalimbali za kubuni biashara mpya,kupanua biashara au soko pamoja na huduma kwa wateja.
Mpenzi msomaji ukweli ni kwamba akili  za kuzaliwa hazitoshi katika kumwezesha mfanyabiashara wa leo kubuni na kuendesha biashara yenye mafanikio.Biashara yenye mafanikio ni biashara ambayo ni mathalani inaweza kuhimili ushindani wa soko huria pamoja na kukuwezesha kurudisha mkopo uliokopa kwa ajiri ya kuanzisha biashara.
Ndugu msomaji katika kubuni biashara mpya ni kwamba mfanyabiashara anatakiwa kubuni biashara ambayo itamletea mafanikio na sio kubuni biashara ambayo itamletea hasara japo katika biashara hasara hazikosekan,pia katika kubuni biashara mpya kinachohitajika ni mawazo yako ambayo yatakupelekea kubuni biashara nzuri ambayo itakuletea manufaa pamoja na kuweza kukua kiuchumi,pia wazo zuri la biashara litakusaidia kujua uzalishaji mali pamoja na kupanuka kimawazo na kiakili.
Katika kupanua biashara ukweli ni kwamba wakati huu ndio wa kufikiri zaidi kiubunufu na kimkakati na suala utakaloamua hapa ndilo litakalokusogeza mbele kibiashara utafiti unasema kuwa biashara nyingi hufa kabla ya kumaliza mwaka mmoja hii inatokana na kushindwa kumiliki ushindani wa kisoko unaosababishwa na wamiliki wa biashara husika kutokana na elimu ya ujasiriamali ambayo ingewawezesha kufanya maamuzi ya busara.
Pia biashara yoyote inatakiwa iwe pana hiini kutokana kuifanya biashara hiyo ijulikane sehemu mbalimbali mfano unaanzisha biashara ya batiki ili biashara hiyo ikue na kujulikana zaidi lazima uwe na vifaa vya kutosha ambavyo vitakusaidia katika kufanya biashara hiyo ikue kwa kuanzisha huduma mpya ndani ya biashara yako na katika sehemu mbalimbali za mkoa au kufungua tawi linguine ili kuipa nafasi biashara yako kufanya kazi katika wigo mpana zaidi.
Katika hatua ya kukomaa biashara inakuwa endelevu pamoja na vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyoweza  kutengeneza faida inayoweza kutoshereza kubuni biashara nyingine mpya tofauti na uliyonayo pamoja na mafanikio hayo mwenye biashara anatakiwa asibweteke badala yake akae na mtandao wa taarifa ili kuifanya biashara mpya kila siku.
Hali kadhalika katika kuipanua biashara au soko mfanyabiashara unatakiwa kuongeza mtandao mfano kuongeza au kupanua soko lako ambapo hapo awali ulikuwa unafanya biashatra yako mkoani Arusha,Tanga,Shinyanga na sehemu nyingine.
Lengo la biashara ni kupata na kutunza wateja na si kupata fedha,ubora na ukubwa wa biashara unaangaliwa kwa wingi wa wateja wa biashara husika.Waswahili husema kuwa ghali kumpata mteja mpya kwenye biashara yako kuliko kumtunza au kuendelea kumfanya mteja wako wa zamani kuendelea kuwa mteja wako.Kwa mantiki hiyo ni kwamba changamoto za biashara za leo ni juu ya kupata wateja wapya kuliko kuendelea kumtunza mteja wa zamani lakini katika hali ya kushangaza si wafanyabiashara wengi wanajihusisha na mambo ya kutafuta wateja wapya bali wengi wanachojali ni pesa tu.
Pamoja na hayo wafanyabiashara wengi wa kitanzania wanafikiri biashara ni sehemu ya kuonyesha ufahari na majivuno bali biashara ni huduma kwa jamii nzima.Mwananchi hebu jiulize unakwenda kununua bidhaa Fulani unamkuta mtoa huduma au mmliki wa bidhaa hizo hana kauli nzuri je utaendelea kununua bidhaa zake ama utauliza na kwenda kwingine?ambako utapata bidhaa hizo kwa mhudumu ambaye anajua kanuni na sheria za mteja.
Mfanyabiashara yeyote mwenye busara atangalia faida ya mteja kwa mtazamo wa muda mrefu na sio mtazamo wa siku moja.Pia mfanyabiashara ambaye anajua wateja wake wanataka nini kwake uwa anapata wateja wengi tena wa kudumu kutokana na huduma yake anayotoa,hivyo mfanyabiashara yeyote anatakiwa awe na mbinu mbadala za kuweza kupata wateja ambao watadumu bila ya kuwapoteza ,wahenga walisema ni heri kupoteza bidhaa kuliko kumpoteza mteja ambaye anakuweka hapo kwa ajili ya kumhudumia.
Mwananchi amka jifunze ujasiriamali ambao utakusaidia kutatua matatizo ya kifamilia pamoja na kupata fedha ambazo zitakusaidia kukuza uchumi wa nchi na kujitoa katika janga hili la umasikini hivyo basi nakushauri acha kusema nimekosa kazi na huku akili umepewa za kufikiri.Hivyo basi ujasiriamali umewatoa watu katika hali duni na hivi sasa ni wafanyabiashara wa kimataifa,mwananchi unatakiwa uache uvivu fanya kazi ili kujikomboa katika janga hili la umasikini ambalo limekuwa tishio katika nchi.
Hata hivyo ujasiriamali ndio kiinua mgongo cha nchi,Ndugu msomaji hebu jiulize kama watu wote wangekuwa hawajishughulishi na biashara ya aina yoyote  je nchi hii ingeenda wapi pamoja na watu wangepata wapi mahitaji yao?Mwananchi amka jipange sasa hivi ni nyakati za kupambana kiume usiku na mchana fanya kazi sababu ukitegemea kuajiriwa serikalini utasubiri sana.hivyo jipange achana na dhana isemayo mie siwezi hakuna mtu katika dunia hiiasiyeweza kufanya kazi wote wanaweza kufanya kazi.
Pamoja na hayo waewza sema ujasiriamali ni ujasiri wa kutafuta mali na usifanya klazio kwa mazoea amka jipange na katika kujipanga neon kukata tama futa katika mawazo yako.
Mwisho  ningependa kukushauri ngugu msomaji wa makala hii jifunze ujasiriamali ambao utakutoa katika janga hili la umasikini na kuwa tegemezi na huku una mikono pamoja na macho,hivyo kumbuka siku zote ujinga ndio wa bei ghali zaidi kuliko bei ya elimu.

Wednesday, September 19, 2012

MAKALA MAALUMU TOKA DAR ES SALAAM


Masuala ya Msingi Katika Mwelekeo Mpya wa Hatima ya Taifa Letu

 

Na Gwandumi Gwappo Atufwene Mwakatobe

Septemba 15, 2012, Mwakaleli (Kandete)

 

1. Itikadi na Falsafa ya Taifa

 

Taifa letu linapaswa kuwa na itikadi na falsafa inayotuongoza na inayoweza kurithishwa kutoka vizazi vilivyopo na vijavyo. Itikadi na falsafa ambayo inalinda utamaduni wetu, utu wetu na maisha yetu kwa kuyapa kipaumbele cha kwanza dhidi ya vitu na mali. Itikadi na falsafa nyingi zilizopo na zilizopita zinalenga mifumo ya uchumi badala ya kujikita katika kulinda heshima na hadhi ya utu wa mtu kwanza. Tumepitia vipindi vya ujima, ujamaa, ubepari, ubeberu na mitazamo inayokinzana kimrengo ambayo yote inahusiana na mali au utajiri wa kiuchumi (material wealth), ambayo haijali utu na maisha ya mtu. Tumesahau kuuendeleza utu, heshima na utukufu alionao mtu bila kujali matabaka ya maisha kiuchumi. Bila itikadi na falsafa inayotuongoza tutakosa utamaduni wetu na tutakosa mwelekeo wa jamii na taifa kwa ujumla.

 

Kwa waraka huu natamka kwamba nchi yetu itafuata itikadi na falsafa ifuatayo:

 

Kulinda, Kuheshimu na Kuendeleza Misingi ya Utu wa Mtu na Maisha Yake Kwanza Kuliko Mali na Vitu.

 

Misingi ya Utu ina mihimili mikuu minne: Huruma, Ukarimu, Kujali na Utumishi wa mtu kwa binadamu wenzake, hususan jamii inayomzunguka na taifa lake. Maliasili au rasilimali zozote zile kama wanyamapori, misitu, maji, madini, fedha, nakadhalika, haviwezi kupewa kipaumbele kuliko utu wa mtu na maisha yake.

 

2. Haki ya Msingi ya Raia

 

Raia yeyote nchini anayo haki ya kushiriki kikamilifu katika kuiendeleza jamii na taifa kwa ujumla kwa kutumia kipaji, ujuzi, utaalamu, maarifa na nguvu alizonazo bila kizuizi chochote. Haki ya kuitumikia na kuiendeleza jamii yako ndiyo haki ya msingi na nguzo ya umoja wa kijamii na kitaifa. Ieleweke kuwa hakuna jamii au nchi yoyote duniani iliyoendelezwa na taasisi au chama cha siasa. Nchi inaendelezwa na raia wake wenye uzalendo na uchungu wa kimaendeleo kwa kutumia tunu zao walizojaliwa na Mungu – si chama cha siasa. Mhandisi, fundi, mbunifu, mkulima, msanii, mtaalamu wa tiba, mwalimu, mwanamichezo, mvuvi, mjasiriamali, mwenye kipaji cha uongozi, nakadhalika; hao ndio huiendeleza nchi.

 

Ukiwa mhandisi huhitaji kuwa mwanachama wa chama cha siasa ili kulijenga taifa lako. Ukiwa mkulima stadi huhitaji kibali au tiketi ya chama cha siasa ili uinue kilimo nchini. Vivyo hivyo ukiwa na kipaji cha uongozi huhitaji kuwa mwanachama wa chama cha siasa ili kuiongoza jamii yetu katika ngazi yoyote ile, mathalani uenyekiti wa kijiji, udiwani, ubunge na hata urais.

Haki ya kiraia ya kutumia kipaji chako kuliendeleza taifa letu ni haki ya msingi ambayo haipaswi kuwekewa kizuizi au sharti la aina yoyote ile. Ni ukandamizaji usio mithilika kumtaka raia katika nchi yake apitie chama cha siasa ili awe mkulima, mhandisi, mganga, mwalimu au kiongozi kwa kushika wadhifa au cheo katika ngazi yoyote ile. Na kwa msingi huo hatusemi huyu ni mgombea binafsi bali ni mgombea kupitia haki yake ya kiraia ilmradi amethibitika kuwa ni raia wa Tanganyika, Zanzibar au Tanzania kwa mambo ambayo yanahusu muungano.

 

3. Kukomesha Ubaguzi na Ukiritimba wa Vyama vya Siasa Ili kujenga Umoja

 

Vyama vya siasa vimenyang’anya kwa muda mrefu haki ya uhuru na ushiriki wa wananchi katika kujiletea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamduni. Tumekuwa tukipiga kelele kwamba ukabila, rangi, udini na matabaka ya watu kimaisha yanaleta ubaguzi na hata uhasama. Lakini vyama vya siasa vimekuwa vikifanya ubaguzi na uhasama mkubwa zaidi na hata kuthubutu kudai serikali ni mali ya chama fulani, wakati kiukweli inatokana na wananchi na ni taasisi ya umma – si chama cha siasa. Chama kinapodai serikali ni mali yake wakati inawekwa madarakani na umma huwafanyi watu wa vyama vingine na wasio na vyama wajisikie kwamba si serikali yao. Wanaona hawana serikali, jambo ambalo tunaona wanaojiita  wenye chama tawala wakipandisha mabega na kujiona wana haki zaidi katika nchi kuliko wananchi wenzao. Ni ubaguzi mbaya unaovunja umoja wetu wa kitaifa kudai serikali ni ya chama fulani. Serikali ni taasisi ya umma, si ya chama cha siasa. Chama ni taasisi au asasi ya baadhi ya watu, si ya umma. Vyama vya siasa vinakuja na kuondoka lakini taifa litadumu daima endapo umoja wa kitaifa utalindwa na kuzingatiwa.

 

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Toleo la 2008, Sehemu ya Pili, ibara ya 8, kifungu cha 1(a), ukurasa wa 23, inabainisha wazi kwamba: “Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii.” Serikali inapata madaraka kutoka kwa umma (wananchi) na si chama cha siasa. Hakuna chama ambacho kiko madarakani isipokuwa kuna serikali ya wananchi iliyoko madarakani. Rais aliyepo ni wa umma si wa chama cha siasa – hakupata madarakani kutokana na chama siasa bali umma uliomchagua kutoka kwa watu wenye vyama na hata wasio na vyama.

 

Tumeona hata bunge linaendeshwa kiubaguzi wakati ni taasisi ya umma ambayo kamwe haipaswi kujinasibisha na vyama vya siasa kwa kuwa hata wabunge/wawakilishi wanatokana na wananchi na si chama cha siasa. Kazi inayofanywa na vyama vya siasa ni kuendesha mchakato tu wa kupata wagombea ambao mwishowe huchaguliwa na wananchi wote kuwa madiwani au wabunge. Tunashuhudia uhasama miongoni mwa wananchi unaotokana na kuegemea chama fulani na kuleta mgawanyiko unaohatarisha au kuvunja kabisa umoja wetu wa kitaifa. Lazima tuwe na masuala tunayokubaliana kitaifa na kuyapa kipaumbele.

 

Ni aibu kuona wanasiasa wakiunganishwa na misiba tu badala ya ajenda na masuala ya kitaifa. Mbaya zaidi ni pale ambapo mbunge akifukuzwa au akikiacha chama chake ananyang’anywa ubunge ambao alipewa na wananchi waliomchagua. Wananchi wananyang’anywa demokrasia yao na mbunge wao. Hii ni dhambi kubwa! Chaguo la wananchi halina budi kulindwa kikatiba na wananchi ndio wanaopaswa kumweka mtu madarakani au kumwondoa. Ipo haja ya kuweka na kuulinda msimamo huu kikatiba.

 

Aidha, chama chochote cha siasa kinachotaka kujijenga kwenye mioyo ya wananchi hakina budi kuacha kujijenga chenyewe bali kishiriki kulijenga taifa na kushughulikia matatizo yanayowakabili wananchi. Si busara kununua gari la kuendeshea kampeni za kisiasa huku zahanati, kituo cha afya au hospitali ikiwa haina gari ya wagonjwa au kuhudumia wajawazito. Chama cha siasa kikiamua kuchimba kisima, kuchonga madawati au kujenga madarasa badala ya kujenga ofisi ya chama kinakuwa kimejiwekea msingi mzuri miongani mwa jamii. Sioni mantiki ya kutumia mabilioni ya pesa kufanya kampeni za kumpata mbunge huku tukishindwa hata kujenga zahanati katika kijiji kimoja. Wala hatuna haja ya kuwa kadi za vyama vya siasa kwa kuwa chama kinapaswa kugusa na kuishawishi mioyo ya watu na matatizo yao hatimaye ndipo hupendwa na kuungwa mkono, na pengine kwa dhati zaidi kuliko wenye kadi. Na kwa kipengele hiki napendekeza Chama Cha Mapinduzi kibadili malengo yake pamoja na jina. CHADEMA kiache kuiga mwenendo wa CCM, na iwe vivyo hivyo kwa vyama vingine.

 

4. Suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

 

Awali ya yote, kama alivyowahi kusema Mwalimu Nyerere kuwa ukimwambia mtu mzima ukweli unamheshimu, lakini ukimwambia uongo unamdharau. Ni kuwadharau wananchi kuendelea kuwaambia kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina serikali mbili. Kusema ukweli tuna serikali za aina nne hapa nchini – na si mbili kama ambavyo wengi wameaminishwa. Serikali hizo ni:

 

  1. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambayo imekuwa wazi sana kiutendaji na kimuundo
  2. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT/URT) ambayo ilianza na masuala 11 wakati wa kuanza muungano mnamo Aprili 26, 1964
  3. Serikali ya Tanganyika ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijificha kwenye masuala ya muungano au kama ambavyo wengine kimakosa wamebuni jina la Tanzania Bara
  4. Serikali za mitaa ambazo zinatenda kazi katika ngazi ya vitongozi, mitaa, vijiji, wilaya, miji, manispaa na majiji.

 

Na ieleweke kuwa Tanganyika na Zanzibar hazikufuta hadhi ya kuwa nchi isipokuwa tu katika masuala ambayo ni ya muungano, na kwa miezi kadhaa baada ya kuungana, nchi ya muungano iliendelea kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi pale ambapo mshindi wa kutunga jina moja la muungano alipounganisha TAN kutoka kwenye herufi tatu za kwanza za Tanganyika na ZAN kutoka kwenye herufi tatu za kwanza za Zanzibar, na kumalizia vifupisho vya majina yake mawili vya I na A na kupata TANZANIA. Unapotaja TANZANIA unataja mambo ambayo ni ya muungano, yanayobaki yanakuwa ya nchi ya Zanzibar upande mmoja wa muungano na nchi ya Tanganyika kwa upande mwingine.

 

Hadi leo hakuna mahali popote ambapo jina Tanganyika lilifutwa na kuwekwa jina lingine. Na hadi leo Hati ya Muungano ndio mkataba pekee ulio hai kuhusiana na muungano wa nchi mbili. Wanaoita Tanganyika kuwa ni Tanzania Bara wanakosea sana kwa kuwa hatujawahi kubadili jina la Tanganyika kuwa Tanzania Bara. Hata tungekubaliana kisheria bado tungekosea kuiita Tanganyika Tanzania Bara kwa kuwa pwani yote (Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Tanga) haiko bara! Aidha visiwa vya Mafia, Songosongo, Koma, Kwale, Ukerewe na kwignineko haviko bara!

 

Nisisitize kuwa, hali halisi na muundo halisi wa kiutendaji uliopo sasa tangu Aprili 26, 1964 ni wa serikali tatu: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Tanganyika ambayo kimakosa inajificha kwa kutumia jina la Tanzania au Tanzania Bara. Pia kuna watu walijitungia kienyeji kwa kubdadili jina la Zanzibar na kuita Tanzania Visiwani bila kujua kuwa hata visiwa vya Ukerewe na Mafia ni Tanzania Visiwani lakini haviko Zanzibar! Na waliendelea kutapatapa tena kwa kuiita Zanzibar Tanzania Zanzibar wakati ni Zanzibar na ndiyo jina lililomo kwenye hati ya muungano. Nashukuru kwamba wazanzibar wameendelea kuiita nchi yao kwa jina la Zanzibar.

 

Nisisitize kuwa mambo yote yasiyo ya muungano yanashughulikiwa au yanasimamiwa na Zanzibar au Tanganyika. Kusema masuala yasiyo ya muungano yanashughulikiwa na Tanzania kwa upande wa Tangayika ni makosa kwa kuwa si ya muungano, maana Tanzania ni kwa ajili ya masuala ya muungano tu! Wenzetu Zanzibar wanakwenda sawia na unavyosema mkataba almaarufu Hati ya Muungano na wako wazi sana katika kufuata mkataba huo na kuulinda.

 

Hadi leo hii tuna sikukuu za aina tatu: uhuru wa Tangnyika wa Desemba 9, mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 na muungano wa Aprili 26. Kimahesabu huwezi kuunganisha vitu viwili ukabakiwa na vitu viwili. Utakuwa na kimoja au zaidi ya viwili! Huwezi kuwaoza mwanamke na mwanaume ukawa na ndoa mbili. Itakuwa ndoa moja tu. Ukiunganisha maumbo mawili yaliyounganika kwa sehemu tu unapata maumbo matatu: kiunganiko (intersection set) na sehemu mbili ambazo hazijaunganika. Kuendelea kusema uongo kwa kudai kuwa Tanzania kuna serikali mbili wakati hali halisi kiutendaji ni serikali tatu ni kuwadharau wananchi.

 

Tanganyika ilikuwa na umri wa miaka miwili na miezi mitano tu ilipoungana na Zanzibar kwa mambo 11 tu (sasa yako 22), tangu ilipopata uhuru Desemba 9, 1961; na Zanzibar ilikuwa na umri wa miezi minne tu na siku kadhaa tangu ilipopata uhuru Desemba 10, 1963, na ilikuwa na umri wa miezi mitatu tu tangu ilipofanya mapinduzi Januari 12, 1964, ambayo ndiyo yanayoenziwa. Leo hii hatuwezi kujigamba kwamba Zanzibar imefaidika na muungano kwa kuwa haikuishi muda mrefu nje ya muungano (miezi mitatu tu) na kuzitumia vizuri fursa za kitaifa na kimataifa. Na Tanganyika pia haikuishi muda mrefu nje ya muungano (miaka miwili tu na miezi mitano). Tanganyika imekuwa ikigharamia mambo mengi ikiwa pamoja na kuwaruhusu Wazanzibar washiriki bungeni kwa mambo yasiyo ya muungano wakati Watanganyika hawashiriki kabisa kwa upande wa Zanzibar.

 

Nihitimishe kwa kusema kuwa suluhisho muafaka na thabiti la kudumisha uhusiano mwema na Wazanzibar ni kuwaachia kabisa wawe taifa huru na dola kamili kitaifa na kimataifa. Tanganyika nayo ibakie kamili ili tuondokane kwa amani na kero nyingi za muungano. Tubakie majirani wema kama ilivyo kwa Zambia, Msumbiji, Rwanda, Kenya na kwingineko. Kuwa na mahusiano mema na jirani ni jambo la msingi na si lazima muunganishe nchi. Kuna nchi nyingi tunahusiana nazo vizuri sana na kwa ukaribu japo haziko jirani. Undugu ni mahusiano mema si kuunganisha nchi.

 

Zanzibar imekosa fursa nyingi za kimataifa kwasababu ya kubanwa na kufinywa na muungano. Kwao muungano ni jinamizi! Si vema kuendelea kuwabana watu ambao ni ndugu zetu kama ilivyo kwa nchi zote jirani. Kuna faida nyingi kwa Tanganyika na Zanzibar kuwa nje ya muungano. Hatuwezi kuendelea na serikali tatu na mifumo tata inayotugharimu fedha nyingi na kero zisizoisha. Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanganyika, na bariki uhusiano wetu mzuri na wa kijadi kati ya Zanzibar na Tanganyika na nchi zingine jirani na zilizo mbali.

RC SINGIDA AWAPA SOMO WAANDISHI WA HABARI


Na HALIMA JAMAL

Singida

MKUU wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, amewataka waandishi wa habari mkoani hapa kuanzisha kikundi cha kuweka na kukopa (SACCOS),ili kujijengea mazingira mazuri ya kukopesheka.

Dk.Kone ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya ofisi yake juzi.

Alisema maisha ya kutegemea mishahara au posho peke yake,uzoefu unaonyesha kuwa maisha hayo kamwe hayawezi kukidhi mahitaji yote muhimu.

Dk.Kone alisema dawa pekee ya kumaliza makali ya maisha, ni kujiunga/kuanzisha SACCOS mahali mikopo ya masharti nafuu,inapatikana.

“Mkianzisha SACCOS yenu,mtavutia taasisi mbalimbali za kifedha kuweza kuwakopesha fedha.Fedha hizo mtazitumia katika kukopeshana kwa ajili ya kuendesha miradi mtakayoianzisha ya kuwaingizia kipato”,alisema mkuu huyo wa mkoa.

Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, aliwataka waige mifano kutoka kwa wafanyakazi wa idara za serikali,makampuni na asasi mbalimbali ambao wameboresha hali zao za kiuchuni kupitia SACCOS zao.

“Chukueni mfano kutoka kwa wafanyakazi wa ofisi yangu wanavyoneemeka na SACCOS yao,sio ofisi yangu tu,hata wafanyakazi wa benki kuu nao wana SACCOS yao.Wafanyakazi wa benki kuu kwa vyo vyote mishahara yao ni mikubwa pengine kuliko yenu.Lakini pamoja na mishahara yao hiyo, wana SACCOS ambayo inawasaidia kujiendeleza kiuchumi”,alifafanua.

Aidha Dk.Kone alisema anaamini kwamba waandishi wa habari wakiwa na hali nzuri kiuchumi,watatekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Aidha,alisema anaamini pia kwamba waandishi wa habari hali zao za kiuchumi zikiwa nzuri,mkakati wa kukuza uhuru wa vyombo vya habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji,utafanikiwa.

“ kweli,niko ‘serious’ na jambo hili,nataka nitakapoondoka mkoani Singida, niache kila mwandishi wa habari,anakuwa na hali ya kuridhisha ya kiuchumi”,aliongeza Kone.

“Ni kupitia SACCOS pekee ndio mtaweza kujijengea nyumba bora,kugharamia masomo ya watoto wenu na mambo mengine yote muhimu kwa maisha”.

Kwa upande wake katibu msaidizi wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,Emmanuel Michael,alimhakikishia mkuu huyo wa mkoa Dk.Kone,kuwa ushauri wake huo wataufanyia kazi mapema iwezekanavyo.

“Kwa kweli hali zetu za kiuchumi haziridhishi kabisa.Kwa kifupi wengi wetu tumepigika kimaisha.Mbaya zaidi ni kwamba tumekuwa tukitumia kalamu zetu katika kuyahamasisha makundi mengine kujikomboa kiuchumi huku sisi wenyewe tukijisahau”,alisema katibu huyo msaidizi.

Emmanuel ambaye ni mwandishi wa habari wa radio free afrika na star tv, alisema ushauri huo wataufanyia kazi ili wafike mahali hali zao za kiuchumi na pia klabu yao iwe na uwezo wa kujitegemea.

 

WATOTO WATEMBEA KM 15 KUFUATA SHULE

Na,Jumbe Ismailly
 
Ikungi, Singida     


WANAFUNZI wa shule ya awali ya Kijiji cha Damaida,kata ya Mkiwa,wilaya mpya ya Ikungi hutembea umbali wa kilomita 15 kwenda na kurudi kufuata masomo yao katika shule hiyo.

Hayo yamebainishwa na mmoja wa walimu wa shule hiyo,Sister Maria Mwiru alipokuwa akitoa maelezo mafupi ya shule hiyo kwa mkuu wa wilaya hiyo,Bwana Manju Msambya aliyetembelea shule hiyo kuona changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Amefafanua mwalimu huyo kuwa mahudhurio ya katika shule hiyo yenye wanafunzi sitini wenye umri wa kati ya miaka 3 hadi 5 ni mazuri sana wakati wa kiangazi lakini yamekuwa mabaya pia katika kipindi cha masika kutokana na watoto hao wadogo kushindwa kutembea umbali huo.
 
Kwa mujibu wa Sir Mwiru kiwango cha mahudhurio wakati wa kiangazi hufikia asilimia mia moja lakini kwa kipndi cha masika hushuka hadi kufikia asilimia hamsini kutokana na wanafunzi kushindwa kutembea kwenye udongo wenye tope la kunata sana.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo,mwalimu huyo wa shule hiyo inayomilikiwa na Wamishenari wa Urusula Mkiwa ameweka wazi kuwa walilazimika kutofunga shule mwezi wa nane ili waweze kusogeza silabasi kabla ya mvua za masika hazijaanza kunyesha.
Hata hivyo Sir Mwiru ameweka bayana baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni kwamba kutokana na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ni watoto wa wafugaji wa jamii ya kabila la kisukuma hivyo wamekuwa wakijaribu kwenda kuwafuata nyumbani kwao na kuwashauri watoto wa wafugaji hao ili waweze kwenda shule.
Aidha mwalimu Mwiru amesisitiza pia kwamba wanapokwama baada ya kutoa ushauri kwa wazazi wa wanafunzi hao ndipo hulazimika kuwatumia askari wa jeshi la mgambo kwenda kuwafuata na kuwatisha tu ila bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili waweze kuhudhuria masomo,jambo ambalo amesema limeleta mafanikio makubwa sana ya mahudhurio.
Shule ya awali Damaida licha ya kutoa huduma ya masomo kwa watoto hao wenye umri wa kati ya miaka 3 hadi 5,vile vile hutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote wanahudhuria masomo,kitendo ambacho kimesaidia pia ongezeko la mahudhuria ya shule hiyo.

WANAFUNZI WATAHADHARISHWA DHIDI YA UKIMWI


Na. Jumbe ismail na Everister Lucas

Singida

 

KATIBU wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Singida amewaasa vijana wanaomaliza masomo ya elimu ya kidato cha nne nchini kujiepusha na maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi kutokana na kile alichodai kwamba dawa ya kutibu bado haijapatikana.

Katibu huyo,Bwana Samwel Olesaitabahu ametoa tahadhari hiyo wakati wa sherehe za mahafali ya 11 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Singida,iliyopo kwenye Manispaa ya Singida.

Amefafanua Bwana Olesaitabahu kuwa idadi kubwa ya vijana wanaomaliza elimu ya sekondari ya kidato cha nne na hata kabla ya kumaliza masomo yao huanza kujingiza kwenye vitendo vya uasherati,jambo ambalo amesema linachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza nguvukazi ya taifa.

Aidha afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia idara ya utumishi ameweka wazi kuwa malevi kwa vijana ni jukumu la wote kati ya wazazi na walimu,na kwamba ni dhana potofu kuwa walimu ndio wenye majukumu ya kuwasimamia wanafunzi hao.

Hata hivyo afisa huyo amebainisha kwamba ili kufanikisha kupata vijana wenye malezi mema ni vyema wazazi kwa kushirikiana na walimu kuwalea kwa uangalifu wanafunzi na kwamba haitakuwa vizuri kazi hiyo ikaachwa kwa walimu peke yao.

Kuhusu suala la nidhamu kwa wanafunzi,Bwana Olesaitabahu amesema suala la nidhamu katika shule yeyote ile ni la utatu kwa maana kwamba walimu,wanafunzi pamoja na uongozi wa shule,hauna budi kuwa na nidhamu ya pamoja kwa lengo la kuleta ufanisi kwenye taaluma.

Hata hivyo akijibu risala ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne katika shule hiyo,katibu huyo amesisitiza kwamba uongozi wa shule hiyo hauna budi kuweka kipaumbele kulingana na changamoto zinazowakabili wanafunzi wa shule hiyo.

Amefafanua huku akitoa mfano wa vipaumbele katibu huyo wa idara ya utumishi aliutaja ujenzi wa uzio wa kutenganisha chuo na shule hiyo ya sekondari.

Hata hivyo hakusita kuushauri uongozi wa shule hiyo kuanza mara moja kuweka mikakati ya kuendeleza shule hiyo,hususani ujenzi wa uzio huo na alitumia fursa hiyo kuwapongeza walimu wanaofundisha shule binafsi licha ya walimu hao kufundishwa na serikali.

Awali katika risala yake,Mkuu wa shule hiyo,Bwana Francis Ibabila amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana katika shule hiyo,lakini bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni kukosekana kwa maabara,maktaba pamoja na uzio unaotenganisha kati ya chuo na shule ya sekondari hiyo.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa shule kukosekana kwa uzio huo unachangia kwa namna moja au nyingine ukosefu wa nidhamu kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Changamoto zingine kwa mujibu wa Bwana Ibabila ni upungufu wa maji ya kutosheleza mahitaji ya wanafunzi pamoja na utoro wa wanafunzi unaosababishwa na ushirikiano mdogo kati ya walimu na wazazi.

Katika mahafali hayo ya 11 jumla ya vijana 56 wakiwemo wavulana 26 na wasichana 30 wamehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Singida,iliyopo katika Manispaa ya Singida.

Tuesday, September 18, 2012

ANNOUNCEMENT


We are happy to announce that, after an interview which took place on September 17, 2012 we have selected 6 candidates between 10 to become new standard Radio FM journalists, as follows

1.   EDSON RAYMOND  from         MWANZA

2.   DORIS MEGHJI                   from          SINGIDA

3.   ABDUL BANDOLA    from          KIGOMA

4.   EUFRASIA MATHIAS from SENGEREMA

5.   EDILITRUDA CHAMI          from SHINYANGA

6.   VERONICA MEDARD        from MANYONI she has been selected to be our Reporter from Manyoni and Dodoma

Please communicate with Radio Project manager for further information as soon as possible

Thanks  

MATOKEO YA UCHAGUZI CCM ILAMBA


Na.  PHESTHOW  SANGA;

 IRAMBA 

Uchaguzi  wa  Viongozi wa ngazi mbalimbali  katika chama cha  mapinduzi { CCM}Wilayani  Iramba  Mkoani Singida umemalizika juzi sept  8Mwaka huu ,Huku  wanawake  wakiwabwaga  chini vibaya  Wanaume  waliogombea katika  nafasi  za Mwenyekiti .

 

Chaguzi  hizozilizoanza  mapema  Septemba 0 4 Mwaka  huu, kwa  Jumuiya  ya Umoja wa  Wanawake Tanzania { UWT}kwa  Jenephar J. Miano , kufanikiwa kutetea  kiti  chake tena,  baada  ya kutangazwa mshindi  na msimamizi  mkuu  wa uchaguzi huo  { mb} wa singida  magharibi mhe  misanga. kwa  kupata jumla ya kura 334 dhidi ya 48 za  Neema Imaryna 31 za Hawa Rajabu.

 

Aidha kindumbwe-ndumbwe  kilikuwepo  kwenye Jumuiya  mbili  za Umoja wa vijana  CCM pamoja na ya Wazazi, katika Jumuiya  yaVijana  Ambapo  wagombea walikuwa watatukatika nafasi yamwenyekiti , wakiongozwa na Ahamed  Makame ,Athumani Rajabu, pamoja na Mwanamke  pekee  Ziyana J.Mtali.

 

Katika Uchaguzi  huoUliofanyika Spt.08 Mwaka huu  ambapokulikuwa  na Upinzani  kubwa kutokana  na wagombea  wote kuwa na Elimu  nzuri Ingawa Athumani Rajabu ,ni mhitimu wa  chuo kikuu Tumaini Iringa,  lakini hawakuweza kufua  dafu baada  ya kusaliti  Amri kwa Mwana Dada, Ziyana Mtali aliyetangazwa  Mshindi na Msimamizi mkuu  Salumu Mkuya ,kwakupata  kura 187kati ya 275zilizo pigwa.

 

Hata hivyo Mapinduzi ya kuwabwaga  Wanaume yaliendeleakwenye Jumuiya  ya Wazazi, ambapo  huko nako wagombea  walikuwa  watatu kati ya hao Mwanamke alikuwa mmoja  pekee Alisimama kuchuana  na wanaume kugombea  nafasi  ya Mwenyekiti .

 

Katika Uchaguzi  huo  Mwana mama ,Monica Samwely  aliibuka mshindi kwa kupata  jumla ya kura 111.kati ya kura pigwa 237 nakuwapiga  chini  Joseph Kidondela  aliyepata  kura 78 na Selemani  Nyamswa aliyepata jumla ya kura 48.

 

Kwa   nafasi  ya wajumbe wa mkutano  mkuu wa  wataifa, { Uvccm }kulikuwa nawagombea wanne  wawili  walishinda ,kati ya hao ni Amri Said,iMhitimu wa chuo kikuu Tumaini Dsm; na Elilumba Reuben .Wakati katikaJumuiya  ya wazazi walioshinda,ni Alberth  Makwala ,Monica Samwely na Rehema Mkassa,kati ya wagombea sita waliojitokeza kugombea nafasi  hiyo.

 

Katibu wa chama cha mapinduzi{ CCM} Wilaya ya Iramba  bwn , Mathias Shidagisha  Akiongea na waandishiwa Habari Ofisini kwake  leo  Asubuhi alisema  kuwa Uchaguzi  umefanikiwa  kwa Aslimia 95,kutokana  na Wajumbe kuhudhuria kwa wingi  ,Ingawa  kulikuwa  na shida  ya Usafiri mkubwa  sehemu  zingine  kutokana na  jiografia ya wilaya kuwa namabonde pamoja na milima mikali.